Home Kimataifa Lionel Messi ndio mfalme wa wafalme

Lionel Messi ndio mfalme wa wafalme

14141
0

Kuna wachezaji kila siku tunaishia kusema “huu ni msimu wake wa mwisho”, “ashazeeka hachukui tuzo wala kombe lingine” kama kuna wachezaji wanaosemwa hivi baasi Messi na Cr7 wanaongoza.

Lakini sasa sikia hii, baada ya kutwaa ubingwa wa Spanish Super Cup mwishoni mwa wiki hii sasa Lionel Messi ndio mchezaji aliyebeba tuzo nyingi zaidi(makombe na binafsi) toka Barca ianzishwe.

Kombe hili la Super Cup linamfanya Lionel Messi kufikisha makombe 33 mbele ya Andres Iniesta ambaye yeye amebeba makombe 32 kwa muda wote akiwa anaitumikia Barcelona.

Ukiacha makombe hayo 33, Messi huyuhuyu katika michezo 638 ambayo ameichezea Barcelona alifunga mabao 552 akatoa assist 239, akabeba kiatu cha dhahabu mara 5 huku tuzo ya Ballon d’or akiibeba mara 5.

Kikombe cha La Liga Messi amebeba mara 9, Super Copa amebeba mara 8, Copa Del Rey akibeba mara 6, Champions League mara 4, klabu bingwa dunia 3 na Uefa Super Cup 3.

Na kama hufahamu tu ni kwamba kabla Lionel Messi hajajiunga Barcelona walikuwa wamebeba makombe 62, Madrid wakibeba 72 lakini baada ya Messi kujiunga Barca wana makombe 95 huku Madrid wakibaki na 92.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here