Home Uncategorized LIVE ( text commentary): Uganda vs Tanzania

LIVE ( text commentary): Uganda vs Tanzania

12719
0

Na mpira umekwisha

Uganda 0-0 Stars

Chilunda amechukua nafasi ya Ulimwengu

Mpira wa kutushwa dakika za lala salama

Dakika ya 94: Bado Ulimwengu hali yake bado sio njema

Hatari Katika lango la Stars Manula anokoa, kessy anaosha. Linapigwa shuti mpira unakwenda nje na inakuwa ahueni kwa Manula.

Thomas ulimwengu yupo chini

Msuvaaaa anapoteza mpira ule

Faulo Ulimwengu anacheza faulo.

90 zimekamilila na zimeongezwa 4

Dakika ya 87: Faulo kuelekea Stars. Waiswa anaenda kucheza faulo ile, Himid Mao anaokoa

Mabadiliko kwa Uganda, Idrissa amechkua nafasi ya Farouk Miya.

Dakika ya 86: Kadi ya Manjano kwa Mudathir Yahya.

Dakika ya 85: kona kielekea Stars, mpira uanokolewa Shambulio la lakushutkiza lakini kipa wa Uganda anaokoa

Stars kadi 2

Uganda kado 3

Dakika 84: Ulimwengu anashikwa na walusimbi. Walusimbi anaoewa kadi ya Njano

Faulo inadakwa na Manula.

Dakika ya 83: Waganda wanalizonga lango la Stars lakini Banda ansimama imara na kuondosha mpira ule. Ulimwengu anacheza madhambi.

Dakika ya 81: Stars wanaelewana vyema lakini shuti la Kesy linakwenda fyongo

Dakika ya 80: Shambulizi ya hatari pale, one two tamu sana ya Samata na kessy lakini mabeki wa Uganda wanasimama imara

Ulimwengu anatolewa nje kwa machela.

Dakika ya 78: Mabadiliko Okwi anatoka anaingia Emmanuel Kizito. Vijibea Banda na Mwantika imemfanya Okwi asifurukute kabisa.

Thonas Ulimwengu yupo chini akigulia maamivu

Mabadiliko. Anatoka Domayo anaingia Himid Mao Nkami Ninjaaa….

Dakika 77: Hassan Kessy anapita na Okwi na inawekwa faulo. Inaonekana huyu mwamuzi anamlinda sana Okwi lakini hamlindi Samata

Dakika 76: Kona kueleka Stars, Unaondolewa na mwantika.

Kipindi cha pili Stars wanaonekana kuelewana.

Dakika ya 72: Msuva anafanya maseke, anapiga bonge la krosi lakini Ulimwengu anashindwa kumalizia

Dakika 71: Aish Manula anawatoa watanzania kimasomaso kwa kuokoa shambulizi la hatari kabla ya Banda kuosha.

Dakika ya 70: Mbagga anatoka anaingia Farid Musa

Dakika 69: Mbwana Samatta anakosa nafasi adimu kabisa yeye golikipa, shuti lake linakoloewa kabla ya chenga yake kukataliwa na kipa huyo.

Dakika 68: Faulo ya Mbwana almanusura Stars wapate goli lakini bao

Dakika 67: Faulo karibu kabisa na eneo la hatari mbwa Samata anavhezewa madhambi. Mita 19

Dakika ya 66: Mabadiliko. Patrick Kabu anaingia kuchukua nafasi ya Ochaya

Mchezaji jezi namba 5 wa Uganda anapasha kuingia uwanjani

Dakika 63: Kepteni wa Tanzania Mbwana Samata anapewa kadi ya manjano

Dakika 62: Murshid anapambana na Msuva lakini anatoa mpira ule nje. Juuko ni mchezaji imara sana

Dakika 61: Shuti la Okwi linapaa mita kadhaa

Dakika 61, Mpira unapigwa kueleka lango la Tanzania Banda anacheza faulo. Faulo inapigwa na ochaya

Dakika 60: Faulo. Mudhathir anamweka chini.

Dakika ya 59: Faulo. Stars wanapata faulo baada ya Msuva kufanyiwa madhambi. Mita 25

Shambulio la kutisha hapa Stars wanapata lakini Wadada anakua makimi na kubloku mpira wa Ulimwemgu aliyekuwa akijaribu kumtafuta Msuva.

David Mwantika anamdhibiti ipasavyo Okwi. Okwi hapumui kabisa.

Faulo kueleka Uganda. Mita 30, Mbwana Samata anatandika bunduki moja matata alamnusura.

Dakika ya 54: Kona kueleka stars. ochaya alipambana na kessy kabla ya kona, mpira unaokolewa na Mudathir, Msuva anajaribu kukimbia kabla ya Wadada kumchezea madhambi.

Dakika 53: Aggrei Morris anaokoa krosi na mpira no wa kurushwa

Dakika 52: Aishi Manula anaokoa katika hatari mbaya sana na yupo chini akionesha kuwa amefangiwa madhambi.

Dakika 51: Kadi ya njano Kw Murshi: Simon Msuva anakimbia na mpira katikati ya uwanja anampa mpira Samatta lakini Murshid anacheza faulo

Uganda 0-0 Tanzania

Thomasi ulimwengu alijaribu kucheza kona ile lakini Onyango alisimama imara.

Dakika 47: Stars inapata faulo. Anaenda kuichonga mpira ule, Mpira unaokolea kisha Gadiel Michael anapiga shuti kali linaokolewa na kuwa kona.

Dakika 46: Krosi ya Okwi inamkosa mchezaji mwenzake baada ya Banda kushindwa kumdhibiti

Dakika 46: Aggrey Morris anaondosha mpira kwenye eneo la hatari lakini anachezewa madhambi na Miya.

Eric Otogo anaashiria mpira kipindi cha pili kuanza.

Uganda wameshiriki Afcon mara 5, Tanzania mara 1.

Wachezaji wanarudi uwanjani. Wachezaji wa Stars wanaonekana kubadilisha jezi zao

Kikosi cha Tanzania hawajafanikiwa kupiga shuti hata moja. Hata hivyo suala la umiliki wa mpira kuwa mbovu ni sababu kwa Stars kushindwa kutulia.

Kipindi cha Kwanza kimekamilika

Uganda 0-0 Tanzania

Waganda wanapata kona

Dakika ya 46: Mudathir Yahya ameshindwa kabisa kuhimili mikikimikiki

Dakika 43: Denis Onyango golikipa wa uganda anatamani apewe gazeti. Jezi yake bado safi..

Dakika 42: Mbwana Samatta anashindwa kuwatoka mabeki wa Uganda na mpira unatoka nje

Bado maelewano ya Ulimwengu na Samatta hayajakaa sawa. Mbwana Samatta ameonekana zaidi kushuka dimba la kati.

Dakika ya 40: Kona wanapata Uganda baada ya shuti kublokiwa na Mwantika

Dakika 39. Uganda wanapoteza nafasi ya uwazi kabisa. Shuti la David Ochaya inakwenda nje, na Kumwacha Farouk Mia akilalamika.

Dakika 38: Aishi Manula anafanyiwa madhambi na wauguzi wanaingia uwanjani kumpatia tiba.

Dakika 37: Hassan Kessy anamchezea madhambi farouk

NB: Waswa anacheza beki, lakini Waiswa anacheza kiungo usichanganye mafaili hapo

Dakika 32: Moses anamchezea Mudathiri ndivyo sivyo. Mpira haujatulia kabisa.

Hali ya uwanja ni mbaya sana. Lakini shuti la Mudathir linakwenda nje kabisa ya lango

Dakika 31: Gadiel Mbagga anachezewa madhambi.

Dakika ya 30: Walusimbi anaisadia sana Uganda kwa upande wa kulia. Mpira wa kurushwa kueleka lango la Uganda anaenda kurusha ni Hassan Kessy

Dakika 29: Abdi Banda anaokoa baada ya Mudathir kufanya makosa. Na Stars wanapata faulo baada ya Msuva kuvutwa.

Dakika ya 28: Msuva anachezewa madhambi mpira bado ni wa nguvu na mgumu sana.

Dakika 28. Farouk Mia anacheza madhambi kwenye lango la Tanzania.

Dakika ya 27: Faulo kueleka Tanzania. Mudathiri amecheza madhambi

Dakika ya 26: Timu ya Uganda inaonekana kuhimili changamoto ya uwanja lakini Watanzania bado wanacheza kwa tahadhari hasa kwa kutumia mipira mirefu.

Dakika 25: Kadi ya njano kwa Lucas Wadada kwa kumchezea madhambi Mbwana Samatta. Faulo inaenda kupigwa na Msuva

Dakika ya 24: Bado ni 0-0 mpira haujatulia.

Dakika 23: Kuelekea lango la Tanzania na ni kona ya 2 kwa waganda lakini unaokolewa na aishi Manula.

Dakika ya 22: mwamuzi anasema ni faulo baada ya okwi kuchezewa madhambi

Dakika 19. Faulo kwenye lango ya Tanzania lakini mpira unazuiwa na kuwa kona kwa waganda.

Dakika 17: Mabeki wa Stars wanakosa umakini lakini Aishi Manula anaokoa mpira.

Dakika ya 16: Denis Onyango anafanya shambulizi la kushtukiza pasi inamfikia Okwi lakini shuti lake linakuwa mboga.

Dakika ya 14: Stars wanacheza vizuri kuelekea lango la Uganda, Msuva pasi yake inablokiwa na Stars wanapata kona ya kwanza

Dakika 10: timu zote mbili zinacheza mpira wa pasi ndefu. Mbwana Samatta anafanya makosa katika lango la Uganda na kupoteza mpira kutokana na utelezi

Dakika 9. Simon Msuva anacheza faulo.

Dakika ya 8. Uwanja una maji Mbwana Samatta anafanyiwa madhambi.

Dakika ya 1. Uganda wanafanya shambulio baada ya mpira wa adhabu kupigwa baada ya mudathiri kucheza madhambi.

Vikosi.

Kikosi chaUgandaCranes.

Masinde_onyango (GK), N Wadada, G alusimbi, Murushid, K Aucho, D Iguma, M Waiswa, Farouk Miya, Emmanuel Okwi, Ochaya, B Joseph.

KIKOSI CHA TANZANIA DHIDI YA UGANDA KUFUZU AFCON 2019

Kikosi cha kwanza cha Tanzania dhidi ya Uganda saa 16:00 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Namboole Jijini Kampala, Uganda, katika kuwania kufuzu Afcon 2019 nchini Cameron.

1:Aishi Manula
2:Hassan Kessy
3:Gadiel Michael
4:Agrey Moris
5:David Mwatika
6:Abdi Banda
7:Simon Msuva
8:Mudathir Yahya
9:Mbwana Samatta (C)
10:Frank Domayo
11:Thomas Ulimwengu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here