Home Ligi EPL London Derby, rekodi zinaibeba Gunners kuipiga West Ham Jumamosi hii

London Derby, rekodi zinaibeba Gunners kuipiga West Ham Jumamosi hii

7128
0

Dstv kama kawaida moto hauzimi wikiendi hii ambapo watakuletea moja kwa moja michezo yote ya ligi kuu nchini Uingereza EPL, moja ya mechi ambazo hipaswi kucheza mbali na remote ya Dstv ni hii London Derby kati ya Arsenal vs West Ham.

Msimu wa mwaka 1954/1955 ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Arsenal kupoteza mechi tatu za mwanzo mfululizo za EPL, tayari wamepoteza 2 za mwanzo wakifungwa na West Ham watavunja rekodi hiyo.

Lakini sio rahisi hata kidogo kwa Arsenal kupoteza mbele ya West Ham, kwani Arsenal katika michezo 22 iliyopita dhidi ya wagonga nyundo hao wa London wamepoteza mchezo mmoja tu katika michuano yote, wakishinda mara 17 na suluhu 4.

Lakini vile vile Arsenal ndio timu ambayo inaongoza kwa kuwafunga West Ham katika ligi kuu ya nchini Uingereza, West Ham wameshakubali vipigo mara 28 kutoka kwa majirani zao hao wa London.

Lakini hayo yasiwape sana matumaini Arsenal kwani ukiacha Man United (8) na Liverpool (7), West Ham ndio klabu inayofuatia kwa kuwafunga Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani (5).

Lakini ni kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya EPL Arsenal na West Ham wanakutana huku michezo yao miwili ya mwanzo ya ligi wote wawili walipoteza.

West Ham wana rekodi mbovu sana katika EPL kwani tangu kuanza kwa msimu uliopita hadi sasa wamefungwa mabao 74 na ndio timu ambayo imefungwa mabao mengi kuliko timu yoyote.

Katika London Derby 9 zilizopita Arsenal hawajapoteza hata moja nyumbani lakininpia msimu uliopita ukiacha Man City, Arsenal walikuwa wanafuatia kwa kukusanya alama nyingi nyumbani na hii inaonesha ubora wao wakiwa nyumbani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here