Home Ligi EPL Macho yote kwa Ole Gunnar leo

Macho yote kwa Ole Gunnar leo

5400
0

Moja ya rekodi wanazoshikilia Man United ni kutokufungwa katika mechi walizocheza uwanja wa nyumbani Siku ya Boxing day ilikuwa mwaka 1978-1979. Mchezo huo walipigwa na Liverpool, kwa mabao 3-0. United wameshinda michezo mara 14 na sare 3.Ole Gunnar kibaruani tena. Jamaa amekuja United na bahati sana. Mechi zake mbili za mwanzo hazina presha sana. Kwa bahati nzuri mchezo wa kwanza dhidi ya Cardiff wachezaji wamecheza kwa kujiamini na wakafanikiwa kupata matokeo.


Utamaduni wa Man United ni wa kushambulia kwa kila namna iwezekanayo. Hatuwezi kucheza kwa kuzia kila mara” Ole Gunnar


Ole Gunnar Solskjser anahitajika kushinda mchezo wa leo ili kuwa meneja wa tano wa Manchester United, kushinda michezo miwili mfululizo ya.Makocha walio wahi kufanya hivyo ni Tj Wallworth, Matt Busby, Dave Sexton, na Jose Mourinho.Leo Manchester United wanacheza na Huddersfield, muda wa saa 18:00 palepale machinjioni Old Trafford.Ole Gunnar ataiongoza Manchester United ambayo imefungwa mchezo mmoja tu kati ya 14 walizocheza na Hudders.Mchezo pekee Untied walifungwa 2-1 Mnamo mwezi October mwaka 2017 ugenini. Ole Gunnar anakibarua cha kuhakikisha rekodi iliyowekwa kwa miaka 88.Ni rekodi ya Hudders kuifunga Man United nyumbani. Mchezo wa mwiso Hudders kuifunga United nyumbani ilikuwa mwaka 1930 mabao 6-0 pale pale OT.United imekuwa na ulinzi imara mara kadhaa walipokutana na Huddersfield. Hudders wamepata wakati mgumu sana wa kufunga bao katika michezo saba kati ya michezo 10, huku wakibahatika kuweka kambani magoli manne tu.


Rooney alinitumia ujumbe akaniambia ni2aache wachezaji wacheze wanavyojisikia. Wasiwe na presha wala wasiwasi. Wafurahie kuichezea Man United

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here