Home Kimataifa Majeraha ya Atletico ndio chanzo cha mikeka kuchanika

Majeraha ya Atletico ndio chanzo cha mikeka kuchanika

11741
0

Diego Simeone amekiri kuwa mzimu wa majeruhi unaiandama sana Atletico Madrid.

Licha ya kikosi cha Atletico kuonekana imara msimu huu lakini bado mambo hayajakaa vizuri. Bila shaka Atletico imechana mikeka mingi sana siku za hivi karibuni. Atletico imeshinda mchezo mmoja kati ya 3 iliyopita ya ligi.

20/08/18 LAL Valencia 1*1 Atlético Madrid
25/08/18 LAL Atlético Madrid 1*0 Rayo Vallecano
01/09/18 LAL Celta de Vigo 2*0 Atlético Madrid

Shida kubwa ni majeruhi

Wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza wamekuwa wakisumbuliwa ana majeraha ya hapa na pale, Santiago Arias (aliumia mbavy), Vitolo (anasumbuliwa na goti), Nikola Kalinic (Uchovu) na Stefan Savic (haematoma na anatumikia adhabu) na hao wote wataukosa mchezo ujao dhidi ya Eibar.

Hata hivyo Angel Correa mwenye shida ya goti pamoja na Juanfran aliyekuwa anasumbuliwa na nyama za paja wamerejea mazoezini ingawa bado hawajakaa sawa.

Kutokana na hali hiyo Simeone imemlazimu kuwajumuisha vijana wadogo Solano na Borja Garces, ambao wote hawajwahi kucheza mchezo wowote wa mashindano.

Lakini Simeone anasemaje?

“Bila shaka kila mtu anaona hali tuliyo nayo, sio njema hata kidogo lakini tunajitaidi kwendana na hali nzima ya klabu kwa sasa,”

“Hatuwezi kukaa chini na kuanza kulalamika, kikosi chetu bado ni imara na tunachokiangalia ni umuhimu wa mashidano haya kwa sasa. Kikosi chetu ni kipana na tuna wachezaji wengi bado”

Mechi za Atletico zijazo

15/09/18 LAL Atlético Madrid 14:00 Eibar
18/09/18 UCL Monaco 22:00 Atlético Madrid
22/09/18 LAL Getafe 19:30 Atlético Madrid
25/09/18 LAL Atlético Madrid 23:00 Huesca
29/09/18 LAL Real Madrid 21:45 Atlético Madrid

“Kikubwa ni sisi kupambana na hali zetu, na nina imani hayo yatapita tu. Ni wakati mgumu sana unapowakosa watu kama Vitolo and Kalinic, sio habari njema kabisa.”

Mchezo wa mwisho Atletico walikuwa kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Celta Vigo, mchezo ambao mashabiki waliishtumu klabu hiyo kwa kucheza chini ya kiwango.


PATA KIFURUSHI

Nilipokuwa Bayern 2016 nilitaka kumsajili Saul Niguez lakini alionekana kuwa ghali sana na bodi ikaamua kumsajili Renato Sanchez” Carlo Ancelotti.

Kiwango cha Saul kimekuwa sana na vilabu vingi vinamnyemelea ikiwemo Barcelona.


Kwa hiyo Simeone kwa sasa ana mpango gani?

“Nakubali lawama zote kuwa timu imecheza vibaya ukiachilia mbali suala la majeruhi. Mimi kama mwalimu nina amini kila mchezaji aliyepo hapa ana umuhimu. Timu inapokosa matokeo lazima mwalimu ubebe jukumu hilo hata kama kuna shida ambayo ipo nje ya uwezo wako”

“Binafsi bado sijavunjika moyo maana kwenye timu yangu kuna ushindani mkubwa Rodrigo na Thomas [Partey], Gelson [Martins] na Correa, [Thomas] Lemar na Vitolo, kiukweli tuwe wavumilivu.”


Kikosi kitakachowavaa Eibar


La liga imetoa takwimu za vilabu vinavyolipa Mishahara mikubwa

Barcelona €632m
Real Madrid €566m
Atletico €293m
Valencia €164m
Sevilla €162m
Villarreal €109m
Real Betis €97m

Ukiangalia tofauti iliyopo katika ya nafasi ya 1 na ya 7 ni kama Real Betis wanaigiza.


Simeone alipoulizwa kama Courtiois ana nafasi kwemye kikosi chake amesema hana nafasi hiyo kwa sababu Oblak ni bora kuliko Courtois, Je wewe una mtazamo gani?


 

Ratiba ya Laliga wikiend hii

14/09/18 Huesca 22:00 Rayo Vallecano
15/09/18 Atlético Madrid 14:00 Eibar
Real Sociedad 17:15 Barcelona
Valencia 19:30 Real Betis
Athletic Club 21:45 Real Madrid
16/09/18 Leganés 13:00 Villarreal
Espanyol 17:15 Levante
Real Valladolid 19:30 Deportivo Alavés
Sevilla 21:45 Getafe
17/09/18 Girona 22:00 Celta de Vigo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here