Home Kitaifa Makala, “Safari ya Ndondo Cup 2018 hadi hatma yake hapo jana”

Makala, “Safari ya Ndondo Cup 2018 hadi hatma yake hapo jana”

6695
0

Usiku wa jana pazia la michuano ya Ndondo Cup 2018 ilifungwa mjengoni Clouds Tv kwa washindi wa michuano hiyo kupewa tuzo zao ambapo tuzo zaidi ya 5 zilitolewa.Kabla ya kwenda kwenda kuzitazama tuzo hizi ni vyema tukaangalia safari nzima ya michuano hii tangu inaanza hadi kufikia usiku wa jana.April 6, 2018 hatua ya awali ya michuano ya Ndondo Cup kwa msimu wa tano ilianza kwa kushirikisha timu 64 kutoka wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam. Kama ilivyo kwa miaka mingine hagua hii huanza mapema ili kupata timu 16 zitakazoungana na timu 16 zingine zilizoingia hatua ya mtoano msimu uliopita na kucheza hatua ya makundi.Kwa ujumla ni timu 80 zimeshiriki Ndondo Cup mwaka huu wa msimu wa tano, hatua ya makundi ilianza June 10 baada ya zoezi la kupanga makundi na utoaji vifaa kufanyika kwa timu zote 32 kama utamaduni wa mashindano haya.Uzinduzi wa hatua hii ulifanyika katika uwanja wa Kinesi, mchezo wa Kundi A kati ya Mabibo Market dhidi ya Keko Furniture ulioshuhudiwa na watu wengi mashuhuri akiwemo Rais wa TFF Wallace Karia, makamu wake, Mbwana Samatta, balozi wa Ndondo Cup Victor Wanyama na viongozi wengine mbalimbali.Usimamizi thabiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) umezifanya timu zilizojiandaa vizuri zaidi kusonga mbele hali iliyosababisha msimu huu kuziona sura nyingi ngeni katika hatua ya robo fainali.Katika timu nane zilizoingia robo fainali zilikuwepo timu mbili tu zilizowahi kuingia hatua hiyo ambazo ni Faru Jeuri na Burudani lakini nyingine zote zilikuwa mpya kwenye mashindano na zingine zikishiriki kwa mara ya kwanza huku wilaya ya Ubungo na Ilala timu zake zikitawala.Pamoja na kuwepo kwa michuano ya kombe la dunia nchini Urusi lakini bado watanzania waliendelea kuthamini cha kwao kwa kuziunga mkono timu zinazotoka katika mitaa yao.Fainali ya tano ya Ndondo Cup ilifanyika August 5 mwaka huu katika uwanja wa Chuo cha Utalii maarufu kama Bandari kwa kwa kuwatanisha mabingwa wa sasa Manzese United dhidi ya Kivule United fainali ambayo iliendelea kuonesha utofauti kila mwaka kwa kumtoa bingwa ambaye ameshiriki Ndondo Cup kwa mara ya kwanza.Msimu wa tano umekuwa na mabadiliko kadhaa yakiwemo ya kombe, medali hata aina ya jezi zilizotumika. Fainali ilihudhutiwa na viongozi mbalimbali wa serikali walioongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, Rais wa TFF, wawakilishi wa makampuni mbalimbali wakiwemo wadhamini wa Ndondo Cup mwaka huu.Kufanikiwa kwa Ndondo Cup hakuwezi kutenganishwa na wadhamini waliojitokeza kuunga mkono jitihada za Clouds, SHADAKA kusimamia mashindano haya na hapo ndipo utawakuta MCheza Tanzania, DCB Bank, Usichukulie poa Nyumba ni Choo na Beko Tanzania, hawa kwa pamoja wametu tukutane jana usiku kupeana tuzo baada ya safari ndefu ya msimu wa tano.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here