Home Tetesi za Usajili Makipa hawa wamevunja benki

Makipa hawa wamevunja benki

12224
0

Chelsea imekalisha usajili wa golikipa wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga kwa ada ya £71 milioni dau kubwa zaidi katika historia ya soka kwa upande wa makipa. Kuna wadau wanauliza imekuwaje Chelsea kutoa dau kubwa kiasi hicho. Bila shaka hawakuwa na namna kwa sabab tayati Thibaut Courtois amekimbilia Real Madrid. Je wangebaki na nani golini? Cabalero? Thubutu…!

Inasemekana kuwa klabu ya Real Madrid itailipa Chelsea £35 milioni (€38.8m, $45m) pamoja na mkopo wa Mateo Kovacic. Courtois alijiunga Chelsea tokea mwaka 2011, alipotokea Genk. Alipelekwa Atletico Madrid, kwa mkopo mpaka 2014. Sakata lake la uhamisho lilianza baada ya yeye kugoma kujiunga Chelsea kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Cobham

Hapa tunaangalia takwimu za usajili wa ghali wa hapo awali wa walinda lango kabla ya Keppa.

Alisson Becker, Roma kwenda Liverpool 2018, £65million

Allison Becker amejiunga na Liverpool msimu huu baada ya Karius kufanya madudu fainali ya UEFA.

GP GC CS MP
Alisson Becker 38 28 17 3,330
David De Gea 38 28 18 3,330

[GP] Mechi [GC:] magoli kufungwa [CS] bila kuruhusu bao [MP] dakika

Mbrazil huyu alijiungaAnfield kwa ada kubwa ya rekodi hapo awali baada Simon Mignolet na Lorus Karius kushindwa kuirridhisha jamii yote ya Liverpool.

Ederson, Benfica Kwenda Manchester City 2017, £35m

Anatoka na Alisson taifa moja. Ederson mwenye 24 aliweka rekoddi ya kununuliwa kwa dau kubwa kabla Allison hajavunja rekodi yake. Bravo alishindwa kumshawishi Pep Guardiola ikabidi waingie mfukoni kumtwaa kijaa huyo.

Gianluigi Buffon, Parma kwenda Juventus 2001, £32.6m

Golikipa huyu mkongwe wa Italia aliweka rekodi kubwa sana wakayi wa usajili wake takribani miaka 17 iliyopita.

Taarifa Binafsi
Majina Gianluigi Buffon
Kuz 28 January 1978 (40)
Mahal Carrara, Tuscany, Italy
Kimo 1.91 m (6 ft 3 in)[1]
No Kipa

Alicheza Turin kwa kipindi cha miaka 17 kabla ya kutimkia Paris St Germain. Buffon amekuwa kwenye ushindani mkubwa sana na Iker Casilas.

Takwimu
M T Mc (G)
1995–2001 Parma 168 (0)
2001–2018 Juventus 509 (0)
2018– PSG 0 (0)

Jordan Pickford, Sunderland kwenda Everton 2017, £30m

Huyu ndiye mchezaji gali zaidi kwa taifa la England akiwa na umri wa miaka 24. Pickford amejizolea umaarufu mkubwa sana Goodison Park kiasi cha kuitwa timu ya taifa England kwenda kombe la dunia.

Takwimu zake timu ya taifa
2009–2010 England U16 5 (0)
2010–2011 England U17 17 (0)
2010–2012 England U18 3 (0)
2012–2013 England U19 8 (0)
2015 England U20 3 (0)
2015–2017 England U21 14 (0)
2017– England 10 (0)

Bernd Leno, Bayer Leverkusen kwenda Arsenal 2018, £22million

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here