Home Kitaifa Mambo 5 aliyozungumza Ndayiragije, awapa tuzo mashabiki

Mambo 5 aliyozungumza Ndayiragije, awapa tuzo mashabiki

2747
0

KMC inawaalika Alliance FC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo, kocha mkuu wa KMC Etiene Ndayiragije amesema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na aina ya mchezo wanaocheza wapinzani wake hivi sasa ukilinganisha na mzunguko wa kwanza.

KMC vs ALLIANCE

“Mechi itakuwa nzuri lakini ngumu kwa sababu sisi baada ya kupoteza mechi ugenini (Lipuli 1-0 KMC) tumeumia lakini tunatakiwa kusahau hayo matokeo ambayo tulipata.”

“Kwenye mchezo wetu na Alliance tutakuwa na wachezaji wetu ambao walikuwa wameumia na bahati nzuri wamejiandaa naimani tutakuwa na kikosi tofauti kidogo chenye nguvu zaidi.”

MZUNGUKO WA PILI UPOJE?

“Kuna wakati nilisema raundi ya pili itakuwa nzuri zaidi kwa sababu angalau timu zimepata nafasi ya kukaa pamoja kwa muda na kuangalia makosa yao kwa hiyo timu ambazo zitaendelea kupunguza makosa na kuongeza ubora wao zitafanya vizuri.”

“Mimi nasema raundi ya pili ni nzuri kwa sababu timu zimejipanga unaona kuna utofauti kwenye uchezaji hakuna tatizo la stamina wala nguvu, wachezaji wanamudu kucheza dakika 90 tayari kumekuwa na uzoefu na watu wamegundua kipi wafanye kupata suluhisho.”

USHINDANI LIGI KUU TANZANIA BARA

“Ligi kuu ina level nzuri kwa sababu timu nyingi zimechukua falsafa ya kuamini vijana na vijana wanajituma na unaona siku hizi timu ikipata pointi tatu inakuwa imezitumikia kweli.”

“Kuna ushindani watu wanajitoa lakini pia siwezi kuacha kupongeza makocha wa timu zote kwa namna wanavyojituma, wanafanya kazi kubwa sana inaleta ladha nzuri kwa wapenda soka. Ni faida kwa nchi kwa ujumla.”

UBORA WA KMC

“Bado hatujafikia kiwango cha kuiongelea sana lakini tumepata vijana wenyeuwezo mkubwa na wana nafasi kubwa ya kuendelea kubadilika na kujiongezea kile wanachohitaji kwenye career yao kwa hiyo tuwape muda tu sisi tunaendelea kuboresha kile ambacho tunakiona ndani mwao ili kiendelee kujitokeza.”

“KMC ni timu ambayo itaendelea kukua siku baada ya siku.”

TUZO YA KOCHA BORA WA MWEZI

“Kwanza nashukuru kwa kupata hiyo heshima lakini siwezi kuacha kuwashukuru na kuwapongeza timu nzima ya KMC.”

“Inaitwa ya kocha bora lakini kwangu naona ni ya timu nzima viongozi, benchi la ufundi na wachezaji ambao tunashirikiana nao kufanya kazi pamoja na mashabiki ambao wapo upande wetu kutupa morali. Tuzo hii nai-dedicate kwa wapenzi wote wa KMC.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here