Home Kimataifa Mambo makuu ya manne ya kutazama mechi za kimataifa, Messi hayupo, Ronaldo...

Mambo makuu ya manne ya kutazama mechi za kimataifa, Messi hayupo, Ronaldo hayupo, Sane karudi kundini n.k

12252
0
Makala hii imeandaliwana Jacob Steinberg, Barry Glendenning na Michael Butler wachambuzi wa jarida la the Guardian.

1) Je Sané atamkosoa Löw ?

Joachim Löw amewaongeza wachezaji wa tatu kwenye kikosi chake. Wachezaji hao ni pamoja na Mchezaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, wa Hoffenheim Nico Schulz na kinda wa  PSG Thilo Kehrer. Ujerumani wakitolewa raundi ya kwanza kwenye makundi ya kombe la dunia tokea mwaka1938. Löw ameamua kurudia matapishi yake kwa kumrudisha kikosini Leroy Sané. Hii ni nafasi yake ya kuonesha kuwa alistahiki kuwamo kikosini wakati wa fainali za kombe la dunia nchini Russia. Ujerumani wapo kundi A la Ligi namba1 ya michuano na UEFA national league. Huu ulikuwa mtazamo wa Jacob

 Alichokisema Samata kuhusu Taifa stars click hapa

2) Zamu ya Luke Shaw

Miaka minne iliyopita Luke Shaw alionekana kuwa mrithi wa Ashley Cole ndani ya timu ya taifa lakini mambo hayakwenda sawa. Mambo hayajaeenda sawa sana  kwa Shaw tokea amejiunga na Man United. Msimu huu Shaw ameanza vizuri kitendo cha kumvutia kocha mkuu wa Southgate na kumjumuisha kwenye timu yake. Huu ni wakati muafaka kwake kuonesha kile alichonacho haswa. Mawazo ya Jacob

 

3) Brazil kumgeukia Richarlison

Richarlison talks to the media at a Brazil press conference in New Jersey.
 

Richarlison amesajiliwa na Everton msimu huu kwa ada ya  £40m akitoka Watford. Ameanza vyema msimu kwa kuwafunga  Wolves na kuipatia Everton ushindi dhidi ya  Southampton. Ingawa hivi majuzi alipewa kadi nyekundu ya kizembe dhidi ya Bournemouth lakini hilo bado halijawazuia Wabrazil kumwamini. Mchezaji huyo mwenye miaka 21 anatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya  USA na El Salvador. Hakuna jipya ambalo Brazil watahitaji kutoka kwake zaidi ya kufunga tu. JS

Mtazamo wa Shaffih dauda kuhusu Antonio Griezmann na Leo Messi kutemwa katika orodha ya wachezaji bora click hapa

4) Ronaldo amkimbia Dalic

“Cristiano Ronaldo ni mbinafsi sana hapendi kuona wengine wanafanikiwa. Siwezi kuwa mchezaji kama yule kwenye timu yangu. Ni mchezaji ambaye yeye moyoni mwake hata timu ifungwe vipi cha muhimu mimi nifunge goli. Hawezi kucheza kitimu kama Modric”

Kwa bahati mbaya Ronaldo amejitoa kwenye timu ya taifa ambayo inatarajia kukutana na Croatia. Stori kamili click hapaMB

5) Dybala kitanzini Argentina

Argentina’s forward Paulo Dybala was little more than a bystander during the World Cup.

Baada ya Messi Higguan na Aguero kushindwa kutwaa makombe matatu ya dunia sasa ni zamu ya Dybala nae kujaribu bahati yake. Kwenye mchezo wa kirafiki dhdi ya Guatemala kocha wa Argentine Lionel Scaloni, Amewatema Lionel Messi na Higuain. Kocha Jorge Sampaoli hakumwamini kabisa   Dybala katika  World Cup. Na huu ni wasaa wake kufanye yake. JS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here