Home Ligi EPL Man United dhidi ya Spurs mtoto hatumwi dukani

Man United dhidi ya Spurs mtoto hatumwi dukani

10799
0
Manchester United wanawakaribisha Tottenham Hotspur
Vikosi vinavyotarajia kuanza
Manchester United (3-4-1-2): De Gea; Bailly, Smalling, Lindelof; Valencia, Matic, Pogba, Shaw; Lingard; Lukaku, Sanchez
Tottenham (3-3-2-2): Vorm; Alderweireld, Sanchez, Vertonghen; Trippier, Dier, Davies; Eriksen, Alli; Moura, Kane
Kwa upande wa Man United wanajivunia baadhi ya rekodi zifuatazo.

Mchezo wa The Reds na the Lilywhites ni moja kati ya michezo inayovutia sana ndani ya ligi kuu England. Kwa upande mmoja mashabiki wa Man United wamekuwa wakiifurahia mchezo zaidi tofauti na watoto hawa wa london. Utakuwa mchezo wa kipekee saba wakati huu Spurs ndani ya Old Trafford siku ya leo watakapotokea kule kaskazini mwa London kwenda kutafuta alama tatu muhimu…

Chevrolet logo

Rekodi za kiujumla
United wamekutana na Tottenham mara 189 tokea mwaka 1899. Timu hizi zilikutana kwa mara ya kwanza kabisa katika kombe la FA Cup ndani ya uwanja wa Asplins Farm, mchezo ulikwenda sare ya 1-1.Man United wamefanikiwa kushinda michezo 89 ikiwa ni sawa na asilimia 47 na mchezo kwenda sare mara 49 huku Tottenhma wakiambulia ushindi mara 51.Jambo zuri kwa Upande wa Man United wanahitaji bao tu ili kufikisha idadi ya mabao 300 dhidi ya Spurs. Kwa upande wa Spurs nao pia mambo si haba kwani wameshaifunga Man United mabao 243.
Takwimu za ligi
Tokea 1992/93 Tottenham ameonekana kuwa kibonde wa Mashetani wekundu. Hii itakuwa mara 53 United kukutana na Tottenham. United wameiadhibu Spurs mara 33 na kwenda sare mara 11 na kufungwa mara 8 tu. United imefanikiwa kutikisa nyavu mara (90) , Tottenham ikijikongoja mara (45).
United pia imewahi kuiadhibu Tott mabao zaidi ya manne katika michezo minne tofauti. Pale White Hart Lane mwaka 2001 na Old Trafford mwaka 2009. Ushindi mwingine ulitokea takribani miaka 100 iliyopita100, Spurs walitandikwa 5-0 kwenye uwanja wa Bank Street 22 Januari 1910. Miaka ile nyota wa Mashetani wekundu kama Charlie Roberts na Billy Meredith waliizamisha Tottenham.

Tottenham pia wanajivunia ushindi mnono walioupata miaka 86 iliyopita walipotoa dozi ya mabao 6-1 mnamo 10 Septemba 1932. William Ridding alifunga bao la kufutia machozi pale White Hart Lane.

Stan Pearson na Norman Whiteside, Shinji Kagawa ns Wayne Rooney, na wachezaji wengine zaidi ya 100 wamewahi kufunga mabao dhidi ya Spurs. Legendi Bobby Charlton na Denis Law wanaongoza kwa kuifunga Tott mabao mengi zaidi wote kwa pamoja wakifunga mabao 15, Law amecheza dhidi ya Spurs mara (19) huku Charlton akicheza mara (38).

Ni wachezaji watano tu katika kikos cha Mourinho ambao wamewahi kuifunga Spurs.

Ashley Young anaongoza kwa kufunga mabao mawili aliyofunga kwenye ushindi wa 3-1 pale White Hart Lane mwaka 2012. Marouane Fellaini alishinda kwenye ushindi wa 3-0 pale Old Trafford mwaka 2015, huku Anthony Martial akikumbukwa kwa bao lake la usiku dhidi ya Spurs msimu uliopita. Alexis Sanchez na Ander Herrera waliiadhibu Spurs kwenye kombel Emirates FA Cup nusu fainali pale Wembley msimu uliopita.

Kuna wachezaji watatu tu ambao wamewahi kufunga magoli matatu kwenye mchezo mmoja dhidi ya Spurs. Willie Bryant alifanya hivyo kwenye ushindi wa 5-3 Denis Law akafanya hivyo United iliposhinda 4-1 mwaka 1963 na Andy Ritchie alifanya hivyo baada ya miaka 17.

Ryan Giggs anashikilia rekodi ya kucheza dhidi ya Spurs mara 42 huku akiwafunga mabao 10. Charlton, amecheza mara 38, na Bill Foulkes mara 33.

Ni wachezaji wanne tu Man United kupewa kadi nyekundu.

Brian Kidd mwaka 1968, United wakipigwa 1-0 kwenye michuano ya FA Cup. Gary Neville alipewa kadi nyekundu miaka 30 iliyofuata wakati wakienda 2-2. Paul Scholes nae akapewa kadi nyekundu lakini United wakapata ushindi wa 3-1 mwaka 2009 na mchezaji wa mwisho ni Rafael da Silva, kwenye suluhu ya 0 bin 0 mwaka 2011.

Manchester United imejifunga mara 6 huku Tott wakijifunga mara 7. Phil Jones alijifunga kwenye kipigo cha 2-0. Mnamo August 2015, Kyle Walker alijifunga

The Reds wamekutana na makocha 28 tofauti wa Tottenham. Lakini bwana Bill Nicholson amekutana na United mara 37. Keith Burkinshaw ni kocha wa pili akikutana na United mara nyingi mara 22 , mwingine Peter McWilliam mara 16. Kocha wa sasa Mauricio Pochettino amekutana na United na klabu mbili tofauti, akiwa na Tottenham na Southampton. Ameshinda mara tatu amepoteza mara sita na kutoka sare tatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here