Home Ligi EPL Man United kujaribu kupata ushindi wa kwanza kwa Brighton baada ya miaka...

Man United kujaribu kupata ushindi wa kwanza kwa Brighton baada ya miaka 76

8960
0

Ligi kuu nchi Uingereza EPL inaendelea hii leo kwa michezo mitatu kupigwa, lakini mechi mbili zinaonekana kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka.

Manchester United ambao mchezo uliopita walishinda kwa bao 2-1 dhidi ya Leicester City katika mechi ambayo United hawakucheza vizuri, laoe watakuwa ugenini dhidi ya Brighton & Hove Albion.

Lakini kama hujui tu hawa Brighton ni wanyonge ila sio kwa Manchester United, katika mechi za Brighton 10 zilizopita katika michuano yote, wameshinda mechi moja na hiyo moja ni dhidi ya United.

Amex Stadium ambao ni uwanja wa nyumbani wa Brighton ni mahala pagumu sana kwa United, katika mechi mbili za mwisho United walizowafuata Brighton wamefungwa zote.

Mara ya mwisho kwa Manchester United kuifunga Brighton katika uwanja wao wa nyumbani ilikuwa mwaka 1942 ambapo alikuwa marehemu Ray Wilikins.

Katika viwanja 58 ambavyo Manchester United wamecheza katika mechi zao za EPL zilizopita wamefunga magoli katika viwanja 56 na ni viwanja viwili tu, hiki wanachoenda leo na Wembley ndivyo ambavyo hawajawahi kushinda.

Katika habari nyingine kuhusu mechi hii ni kwamba wakati Paul Pogba akitarajiwa kuvaa kitambaa cha unahodha hii leo, Alexis Sanchez hajasafiri na timu kuwafuata na Brighton na ilitarajiwa leo asubuhi anaweza akawasili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here