Home Kimataifa Man United yamfukuzia beki wa Spurs

Man United yamfukuzia beki wa Spurs

11832
0

Klabu ya Newcastle United, inakaribia kumsajili mshambuliaji wa West brom wich na timu ya taifa ya Venezuera, Solomon Rondon kutoka West bromwich. Vilabu viwili vya Westbrom na Newcastle vimekuwa vikijadili dii la Rondon mwenye umri wa miaka 28, na dili hilo linaweza kukamilika mwishoni mwa wiki hii. Rondon hakujumuishwa kwenye kikosi cha Westbrom kwenye mechi yao ya ufunguzi ya Championship dhidi ya Bolton jana Jumamosi. Rondon alifunga magoli 7, Msimu uliopita akiwa na Westbrom iliyoshuka daraja msimu uliopita. Kocha wa Newcastle United, Rafael Benitez, amekuwa akitafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi chake, na Rondon anaweza kuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Newcastle msimu huu.

Bournemouth imekubali rekodi ya klabu ya paundi milion 25, kwa kiungo wa Levante, na timu ya taifa ya Colombia Jefferson Lerma. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, alicheza mechi nne za Kombe la Dunia zilizofanyika Nchini Urusi, ilikiwemo mechi waliyotolewa na England kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika hatua ya 16 bora.

Toby anakaribia kutua Manchester United. Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za kumsajili beki wa kati wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Ubelgiji Toby Alderweireld. Taarifa kutoka Daily Mirror zinasema kwamba Manchester United wanatarajia kukamilisha usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 29, ndani ya saa 48 zijazo kwa ada ya Pauni Milioni £60m. Manchester united pia wameripotiwa kutaka kumsajili winga wa Chelsea na Brazil Willian huku wakitaka mabadilishano kati ya Martial na winga huyo mwenye umri wa miaka 29.

Kiungo wa klabu ya Real Madrid, na timu ya taifa Ujerumani Toni Kroos, amechaguliwa mchezaji bora wa timu ya taifa Ujerumani, kwa mara ya Kwanza kwa mwaka 2018. Kroos, mwenye umri wa miaka 28 alipata kura 185 zilizopigwa na watu mbali mbali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here