Home Kimataifa Man United yamlipa Mourinho Tsh bilioni 45, Lovren apatwa maswahibu, Chelsea yapigwa...

Man United yamlipa Mourinho Tsh bilioni 45, Lovren apatwa maswahibu, Chelsea yapigwa mkwara

4987
0

Manolo Gabiadin amekamilisha dili lake kutoka Southampton na kwenda klabu ya Sampdoria.


Imeripotiwa kuwa Manchester United ilimlipa fidia ya £15m zaidi ya shilingi Bilioni 44 kocha Jose Mourinho, baada ya kumfuta kazi Disemba 18, 2018. Mkataba wake katika timu hiyo ulikuwa unamalizika msimu wa 2019/20.


Valencia imethibitisha kuwa Michy Batshuayi atamaliza mkopo wake mapema na kurudi Chelsea mwezi huu.


Msimamo wa London Derby 2018-19 ⚽️

Alama 13 – Arsenal
Alama 13 – ChelseaFC
Alama 12 – SpursOfficial
Alama 7 – West Ham Utd
Alama 4 – Crystal Palace FC
Alama 0 – Fulham FC


Wikiendi hii london derby: 📺 West Ham v Arsenal


Meneja wa Bournemouth Eddie Howe amesema wanaomtaka Callum Wilson wasahau. Kocha huyo amepiga mkwara kuwa mchezaji huyo hauzwi. Wilson anawindwa sana klabu na Chelsea


Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Thomas Muller, ataikosa michezo miwili ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya, baada ya konyeshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Ajax.

Mshambuliaji huyo alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu beki wa klabu ya Ajax, Nicolas Tagliafico.

Nyota huyo ataikosa michezo miwili ya hatua ya 16 wakati miamba hiyo wa Ujerumani Bayern Munich, itakavocheza na Liverpool, hapo mwezi ujao.


Beki mahiri wa klabu ya Liverpool Dejan Lovren hatukuwepo kwenye mchezo ujao dhidi ya Brighto. Hata hivyo taarifa njema ni kurudi mazoezini kwa beki wao wa kati Joe Matip.


Mchezaji wa zamani wa timu ya Tp mazembe Robert Kidiaba ameshinda Ubunge katika jimbo la Upper katanga Lubumbashi.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here