Home Uncategorized Manchester United tabu iko pale pale

Manchester United tabu iko pale pale

9744
0

Ukiangalia namna ambavyo Chelsea, Liverpool au Man City namna wanavyocheza mpira halafu ukawaona United huwezi kuamini kuwa ni United ile ambayo iliteka dunia enzi za Ferguson.

Kabla ya mchezo wa leo kuanza kuna shabiki wa United aliniambia siku izi kila mechi ya United ni ngumu na hakuna timu rahisi kwao na kweli leo tumeona timu iliyopanda daraja mwaka jana ikiwaumbua.

United hawa hawa ambao mechi iliyopita dhidi ya Leicester City walionekana hawajui hata wanachofanya uwanjani na leo tatizo lile lile wanaonekana kuwa nalo wanakufa 3-2 mbele ya Brighton.

Ubovu wa United umepelekea hadi David De Gea kuanza kuonekana kimeo, tangu kuanza kombe la dunia hadi sasa katika mashuti 14 yaliyopigwa langoni mwa De Gea ni mashuti 4 tu aliyookoa na 10 yamekwenda langoni.

Hadi half time tayari Brighton walikuwa na magoli matatu na hii ni mara ya 10 katika historia ya Manchester United kwenye EPL kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa wamefungwa mabao 3.

Japo wamefungwa lakini bao alilofunga Lukaku leo linamfanya kuwahi kuzifunga timu 18 zilizoko EPL msimu huu, na ni Wolves na Cardiff ndio timu pekee ambazo hajawahi kuzifunga.

Katika siku ya leo EPL imeshuhudiwa mabao 16 yakifungwa na ni mara ya kwanza katika historia ya ligi hiyo kwa mechi chache hivi lakini kutoa magoli mengi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here