Home Ligi EPL Manchester United wakaa kileleni mwa ligi kuu EPL

Manchester United wakaa kileleni mwa ligi kuu EPL

11239
0

Iliwachukua dakika mbili tu Man United kupata bao la kuongoza kupitia kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Leicester kuunawa mkono na Paul Pogba kuiandikia United bao la kwanza.Bao la Pogba linawafanya Leicester kuruhusu bao katika michezo yao yote ya ufunguzi katika misimu mitatu ya ligi kuu Uingereza EPL iliyopita.United sasa wanakuwa hawajawahi kupoteza mechi ambayo walitangulia kufunga goli kwenye michezo 122 ya EPL ambayo timu hiyo ilicheza katika uwanja wa Old Traford.Luke Shaw aliifungia Manchester United bao la pili ambapo hili ni bao la kwanza kwa Shaw kuifungia Manchester United katika michezo 67 ya mashindano mbalimbali iliyopita.Lakini kama hujui tu nikukumbushe kwamba katika mechi zote 11 za EPL ambazo Paul Pogba aliifungia Manchester United zilimalizika kwa timu hiyo kuibuka na ushindi.Dakika ya 92 ya mchezo Jamie Vardy aliiandikia Leicester City bao pekee katika mchezo wa leo na kuufanya mchezo kuisha kwa United kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 2-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here