Home Ligi EPL Manchester United wataja kikosi chao cha Champions League, majina ya Rashford na...

Manchester United wataja kikosi chao cha Champions League, majina ya Rashford na Darmian hayapo

17564
0

Klabu ya soka ya Manchester United imetangaza jeshi lao kamili ambalo linakwenda kupambana katika michuano mikubwa barani Ulaya ya Champions League.

Katika majina ya ambao hawapo ni mlinzi wa klabu hiyo Matheo Darmian ambaye katika dirisha lililopita la usajili kulikuwa na taarifa zinazomhusisha na kuondoka katika klabu hiyo.

Tangu msimu huu wa EPL uanze Darmian alicheza mchezo wa kwanza tu wa United vs Leicester ambapo alicheza dakika zote 90 lakini baada ya hapo hakuwahi kuwepo tena katika kikosi hicho.

Badala yake United wamemtaja Diogo Dalot katika kikosi hicho, Diogo alisajiliwa na Man United katika dirisha lililopita la usajili akinunuliwa kutoka FC Porto, na hii kuwa dalili kubwa ya mwisho wa Darmian kuitumikia United.

Marcus Rashford pia hayupo katika list ya wachezaji wa United waliorodheshwa kwa ajili ya Champions League lakini yeye ni kutokana na umri wake.

Kwa sheria za Champions League mchezaji ambaye amezaliwa tarehe 17 January 1997 au baada huwa anaweza kuchezea timu yake katika michuano hiyo hata kama jina lake halipo kwenye orodha A ya majina yaliyowasilishwa UEFA.

October 19 United wataanza kampeni yao ya kuusaka ubingwa wa Champions League watakapowavaa New Boys kabla ya kwenda kukutana na Valencia.

Manchester United hawajawahi kupita katika hatua ya robo fainali tangu mwaka 2011 walipopoteza kwa mabao 3-1 vs Barcelona katika fainali ya michuano hiyo.

Kikosi kamili cha United kwa ajili ya Champions League ni

Makipa : David De Gea, Lee Grant, Sergio Romero

Walinzi : Victor Lindelof, Eric Bailly, Phil Jones, Chris Smalling, Marcos Rojo, Diogo Dalot, Luke Shaw, Antonio Valencia, Matteo Darmian

Viungo : Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Andreas Pereira, Fred, Ashley Young, Ander Herrera, Marouane Fellaini, Nemanja Matic, Scott McTominay

Mafowadi : Alexis Sanchez, Romelu Lukaku, Anthony Martial.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here