Home Kitaifa Maombi yangu kwa CAF, CECAFA na TFF

Maombi yangu kwa CAF, CECAFA na TFF

7756
0

Nilitazama michezo yote miwili ya mshindi wa 3 na ule wa fainali. Nilichogundua kila kocha aliisifia Serengeti boys.Kocha wa Uganda alikiri waziwazi kuwa kikosi cha Tanzania kimejengeka. Ni imani yangu tutamkumbuka sana Kim Poulsen ambaye aliwaandaa vijana hawa tokea wakiwa na miaka 13. Kocha wa Rwanda nae amesema amejivunia sana kuwaona watoto hawa wakicheza na anatamani kuwaona au kuwasikia mbali.Aliongeza kwa kusema serikali ya Tanzania inapaswa kuwasaidia vijana.

Nilibahatika kuongea na wachezaji kadhaa akiwemo Kelvin John. Moja ya swali nililokumbuka kumuuliza ni kuhusu mchezaji mwenzao wa Leicester City ambaye ilisemekana yupo nchini.

“Yupo na sisi (Benny) lakini wakati majina yanapelekwa yeye alikuwa hajajiunga na sisi na jina lake lilichelewa kupelekwa”

Ikabidi nimtafute mwenyewe kwa bahati nzuri nikaonana nae. Kwa maelezo yake anasema anacheza Leicester City ya vijana ya nchini Uingereza. Na alinieleza kuwa amesajiliwa kabisa.

“Wazazi wangu wapo mjini Leicester na tumeishi huko kwa kipindi kirefu. Mimi nilijiunga na Leicester City ya watoto wadogo nikiwa na miaka 11. Kwa sasa nina miaka 16”

Nilimdadisi kuhusiana na utamaduni wa kitanzania kama anauishi au laha akanijibu

“Kiswahili nakifahamu lakini kidogo sana. Nafahamu mambo mengi ya Tanzania ingawa siwezi kusema najua kila kitu”

Pia akaongeza kuwa sababu ya kuchelewa ilisababishwa na maumivu na taarifa kuchelewa kumfikia.

“Nilishindwa kujiunga na timu mapema kutokana na majeraha ya nyama za paja”

Kuhusiana na aina yakr ya uchezaji alisema

“Nafasi ninayocheza uwanjani ni nafasi ya beki wa kulia pia naweza kucheza beki wa kati na kiungo pia”

Baada ya hapo pia nilibahatika kuongea na Morice mmoja ya viungo walionesha kiwango maridhawa. Hakuwa na mengi sana ila anaomba watanzania tuwape sapoti kubwa katika kuhakikisha wanatimiza ndoto zao.

“Natamani kufika mbali. Watanzania wasikate tamaa kutuamini bado tuna nafasi ya kuwarudisha imani hiyo”

Vijana hawa wanaonekana kweli wana morali ya kutosha. Shida ndogo ambayo nimeiona ni kutoka kwenye vilabu vyetu vikubwa Simba na Yanga ambao katika kikosi cha kwanza na wale waliokuwa benchi hakukuwa hata na mmoja aliyetokea Akademi zao. Sio mbaya sana lakini wanapaswa kuhakikisha jungu lao hakikosi ukoko.Pia nmejaribu kufuatilia nchi ya Uganda ambayo inasemekana ina vituo zaidi ya 92 vya watoto. Sisi ni vituo vichache sana kama vile Alliance ambavyo vimezalisha watoto kadhaa akiwemo Kevin John. Ni jambo la kuwapongeza ingawa sifa bado hazina faida kubwa kama tutashindwa kuinua vipaji hivi kufika mbali.

Natamani CECAFA ifike mahali wao pia wasiishie kuanzisha mashindano halafu wapotee. Nilitarajia kusika kuwa watatoa ofa kwa vijana wawili watatu kwenda kufanya majaribio nje. Tulitarajia watengeneze kombania ya kikosi bora ambacho kitawakilisha labda kwenye mashindano mbalimbali ya hisani. Maana asilimia kubwa ya vijana hawa baada ya mashindano haya ndio basi tena. Lengo la haya mashindano sio kushindana ila ni kuinua vipaji. Je kwanini wasiweke mfuko maalumu labda kutoka kwenye akiba ya mashirikisho husika kuweka bajeti ya kitu kama hiki?Tungesikia mtu kama yule Mfungaji bora Mintesnot Wakjira kutoka Ethiopia, au Kevin John pamoja na nahodha bora Morice wangepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio nje.

Pia hili ni jukumu la TFF kuhakikisha vijana wale wanapata fursa nje ya taifa. Ni kwanini kila mwaka wachezaji wanakwenda nje kwa majaribio hatujawahi kusikia mchezaji bora wa Ngorongoro au Serengeti ameenda Standard Liege kufanya majaribio kwa msaada wa TFF?

Hebu tufunguke kidogo. Tufanye jambo la Mbolea. Tusiishie kumwaga sifa tu mwisho wa siku vijana wanapotelea mtaani. Kumbukeni tumekuwa na wachezaji wengi wenye vipaji vya uhakika lakini wamekwama.

Nimejiuliza kama waandaaji wa Ndondo Cup wameweza kumpeleka mchezaji bora wa miaka 15 kufanya majaribio ndani ya Besiktas TFF mnashindwa au kukwama wapi?Tupende kuulinda urithi wa taifa letu kisoka ili tudumishe lulu yetu. Miaka ya nyuma niliwahi kusikia kuhusu kombania ambapo baadhi ya nyota wa Tanzania kama Maulid Dilunga alikuwepo kwenye kikosi cha Afrika All stars na walikwenda mataifa mbalimbali kucheza mechi za hisani. Je CECAFA hawaoni umuhimu wa kutengeneza kikosi bora cha mashindano na kukiwasilisha CAF ili CAF nao watoe maoni yao? CAF wanajukumu la kuinua soka letu na sio kusimamia mashindano tu na hii ni moja ya mbinu ya kusukuma soka la Afrika kwenda mbeleNilitegemea kusikia CECAFA ina bodi ya maskauti wake ikiwa na lengo kupeleka vijana kwenye michakato ya kufanya majaribio. Tusiihie tu kusema Kevi Noma, Morice hatari halafu wanarudi mtaani.. Hapana.. Ahmed Ahmed na mh Rais Karia wanapaswa kukaa chini na kujua ni kivipi watawaendeleza vijana hawa. Asante

Naitwa Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here