Home Dauda TV “Mapinduzi Cup, SportPesa, HAIKUWA TARGET YANGU”-Kocha Simba

“Mapinduzi Cup, SportPesa, HAIKUWA TARGET YANGU”-Kocha Simba

3509
0

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema mashindano ya Mapinduzi Cup na SportPesa hayakuwa kwenye mipango yake.

Mipango yake ni kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa Afrika ambapo Simba imecheza mechi mbili imeshinda moja na kupoteza moja, bado ina mechi nne kwenye Kundi D. Pia amesema nguvu nyingi ataelekeza kwenye ligi kuu ambayo inaweza kuwapa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao.

“Niwe mkweli kwenu, Mapinduzi Cup na SportPesaCup unaweza shinda makombe halafu habari ndio imeishia hapo.”

“Malengo yetu ni Caf Champions League ambapo tayari tumefikia lengo na sasa bado tuna michezo minne, lengo jingine ni kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Tanzania kwa sababu itatusaidia kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.”

“Haya mashindano mengine tunatakiwa kucheza mechi tatu ndani ya siku sita, wakati mwingine tunapaswa kufikiria usalama wa wachezaji!!

“Tulicheza ili tuwe mabingwa lakini tulikuwa tunafanya rotation kwenye kikosi kuwaumiza wachezaji kama unataka kucheza mechi mfululizo kwa kuchezesha kikosi bora kila mechi unaumiza wachezaji na mimi hilo halikuwa lengo langu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here