Home Kimataifa Mario Balotelli aibuka na jipya, achelewa mazoezini lakini arejea na kilo 100

Mario Balotelli aibuka na jipya, achelewa mazoezini lakini arejea na kilo 100

17911
0

Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa na mjasili haachi asili hii ni ukiwaza alichochanya moja washambuliaji watukutu ulimwenguni Mario Balotelli.

Sasa wakati Mario Balotelli klabu anayoichezea ya Nice alichelewa kufika mazoezini na akafika baada ya wiki 2 wakati wakifanya mazoezi ya msimu huu wa Ligue 1.

Watu wa karibu na Balotelli wanasema sababu ya kuchelewa mazoezini kwa wiki mbili ni kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyoipata mwanzoni mwa ligi akawa anaona ni bora asiende mazoezini.

Lakini pamoja na kurudi mazoezini baada ya wiki mbili, Mario Balotelli alikutwa akiwa na kilo 100 wakati kilo zake halisi za siku zote huwa ana kilo 88.

Mario alikuwa na kiwango kibovu wakati wa mchezo wa Italia zidi ya Poland, hali hii ilimpelekea kocha Roberto Mancini kumuacha nje katika mchezo wao uliofuata zidi ya Ureno.

Kwa matukio haya mawili kocha wa klabu ya Nice ameamua kumuadhibu mwanasoka huyo kwa kumkata sehemu ya mshahara wake(haijawekwa wazi ni kiasi gani).

Klabu ya Nice ambayo kocha wake mkuu ni nyota wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira hii leo watakuwa nyumbani katika muendelezo wa Ligue 1 wakiikaribisha Rennes.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here