Home Entertainment Mashabiki wa Ronaldo na Lionel Messi, msikilizeni Gabrielle Union alivyowachana

Mashabiki wa Ronaldo na Lionel Messi, msikilizeni Gabrielle Union alivyowachana

11086
0

Unamjua Gabrielle Union? Nyota wa movie inayotrend sana hivi sasa inayokwenda kwa jina la Breaking In lakini vile vile alikuwepo kwenye movie maarufu ya mambo ya mahusiano iitwayo Think Like A Man (1&2).

Gabrielle pia ni mpenzi wa nyota mkubwa wa kikapu ncbinu Marekani Dwayne Wade na mwezi uliopita tarehe 30 walikuwa wakisheherekea anniversary ya miaka 4 ndoa yao.

Sasa bwana jana baada ya ushindi wa mwanadada Naomi Osaka katika michuano ya Us Open, Gabrielle alijitokeza mtandaoni na kutoa sifa kem kem kwa Serena na Osaka.

Na katika pongezi hiyo alimtaja Serena Williams kama mwanamichezo bora kuwahi kutokea duniani. Baada ya tweet hii kama kawaida mashabiki wa Messi na Cr7 wakaibuka kwenye comments.

Moja ya shabiki wa Messi alienda mbali na kumuambia Gabrielle kwamba amekosea kutaja akimaanisha hakupaswa amtaje Serena kama mwanamichezo bora kuwahi kutokea bali alipaswa amtaje Lionel Messi.

Gabrielle akaona hawezi kuwaacha hivi hivi mashabiki wa Lionel Messi akamjibu kwa kumuambia “siku Messi akijifungua kwa tabu hadi akakaribia kupoteza maisha na akarudi tena kutawala uniambie”.

Jibu hili la Gabrielle lilitokana na tatizo ambalo Serena alilipata wakati akijifungua mtoto wake anaejulikana kama Olympia ambapo wakati wa kujifungua alipata matatizo makubwa kiafya yaliyokaribia kuchukua uhai wake.

Lakini pamoja na tishio hilo la kuumwa sana Serena alifanikiwa kurejea katika tennis akiwa na kiwango kile kile, na hii ndio inamuaminisha Gabrielle kwamba Serena ndio mwanamichezo bora kuwahi kuonekana duniani.

Unaamini kuhusu alichosema Gabrielle na sababu zake?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here