Home Kitaifa Mashabiki Zanzibar wanataka kujua tatizo Yanga

Mashabiki Zanzibar wanataka kujua tatizo Yanga

9336
0

Baada ya Yanga kuendelea kufanya vibaya kwenye mashindano ya kombe la shirikisho Afrika, mashabiki wa timu hiyo visiwani Zanzibar wamekutana kutaka kujua mbali na hali mbaya kiuchumi kunatatizo gani jingine?

Katibu wa matawi ya Yanga Zanzibar Hatibu Kofi ameeleza lengo la kikao chao.

“Tulikuwa na kikao kidogo tukijaribu kuzungumzia masuala ya timu yetu ya Yanga hususan mambo ya usajili na mambo yanavyokwenda kwenye uendeshaji wa timu.”

“Kipindi hiki tunachopitia ni kigumu, ni kipindi ambacho hatujakizoea sana sasa kauli za viongozi wetu wakati mwingine huwa hazitupi matumaini kwa sababu kila mmoja ana lake huyu anasema hili yule anasema lile.”

“Tumekuja kujadili kauli za viongozi halafu tuje na msimamo mmoja kama wanayanga Zanzibar tunafanya nini? Halafu tutawasiliana na viongozi.”

“Kiwango cha timu yetu sasa hivi sio kizuri, tumecheza Kenya na Gor Mahia tumefungwa 4-0 tumerudi nyumbani tumefungwa 3-2. Ni matokeo mabaya sana kutokea katika misimu 10 ya hivi karibuni, ni vitu ambavyo wazanzibar hasa wanayanga vinatuumiza.”

“Viongozi wetu watuambie tatizo letu ni nini? Tunajua hatuna pesa lakini kwa hawa wachezaji waliosajiliwa wanatunzwaje, wanapataje stahiki zao ndio mambo ambayo tumejadiliana na kuona tunafanyaje.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here