Home Ligi EPL Matatizo makubwa 5 ambayo yasipopatiwa tiba United mtaendelea kulia

Matatizo makubwa 5 ambayo yasipopatiwa tiba United mtaendelea kulia

12809
0

Hali sii hali ndani ya klabu ya Manchester United, matokeo mabovu, kiwango kibovu vimeacha klabu hiyo kongwe nchini Uingereza kuwekwa kitimoto kwa sasa.

Kila mtu anaongea lake analoliona kwa sasa, ila ukiiangalia Manchester United kwa sasa haya yafuatayo yanaweza kuwa matatizo makubwa zaidi yanayowaandama.

1.Hakuna ulinzi salama. Tangu kombe la dunia, David De Gea ameokoa mashuti manne tu kati ya 16 ina maana 12 yameenda nyavuni, huyu ukumbuke alikuwa kipa bora EPL katika msimu wa ligi uliopita.

Mou alilalamika wakati wa usajili kuhusu kuhitaji mlinzi wa kati, jambo ambalo halikufanyiwa kazi, hadi sasa United wameruhusu mabao 7 katika mechi 3 tu za EPL.

2.Ushambuliaji butu. Sasa pata picha timu inakuwa na ulinzi ambao sii salama halafu washambuliaji wanatakiwa waibebe timu lakini nao wanakuwa butu, unakwepaje kilio hapo?

Msimu uliopita kwa mfano, United alifunga mara 10 katika mechi 3 za mwanzo, Martial, Rashford na Lukaku walikuwa na mabao 6 wakati kama huu lakini hadi kati ya hao wote kuna bao moja tu ambalo lilifungwa na Lukaku vs Brighton.

3.Chumba cha kubadilishia nguo. Iko wazi kwamba hali ya Manchester United katika vyumba vya kubadilishia nguo sio nzuri hata kidogo na Mou ana tatizo na baadhi ya nyota wa klabu hiyo.

Anthony Martial alimvuruga Mou wakati wa Pre Season lakini pia uhusiano wa Paul Pogba na Mourinho kwa kipindi hiki unaleta hali ya sintofahami katika dressing room ya United.

4.Hajui Xi yake hadi hivi sasa. Kocha Jose Mourinho katika mechi 3 za kwanza United ameonekana wazi kwamba hajui kikosi haswa kinachopaswa kuanza na hadi sasa hajajua mbinu sahihi.

Mfano, katika mechi mbili za mwanzo za United walitumia wachezaji 22 tofauti na mifumo miwili, huku vs Tottenham akajaribu tena 3-5-2 akimuamini Herrera kukaba, ikamfanya Moura kuonekana kama Messi na United wakaangukia pua.

5.Ed Woodward. Pengine hilinlilipaswa kuwa la kwanza, United wanakosa mtu sahihi anayejua soka linapokuja suala la kufanya usajili na aliyepo (Woodward) amekuwa akitofautiana na nini kocha anataka.

Unaweza kumlaumu Mourinho kwa kinachoendelea United lakini kwa matatizo haswa ya ulinzi lawama anatupiwa Woodaward baada ya kutotoa masaada kumnunua beki kama Mou alivyotaka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here