Home Ligi BUNDESLIGA Matokeo, ratiba, ligi 5 bora Ulaya

Matokeo, ratiba, ligi 5 bora Ulaya

3592
0

Kama kawaida michezo ya ligi kubwa barani Ulaya inaendelea weekend hii baada ya kushuhudia michezo kadhaa ya michuano ya ligi ya mabingwa pamoja na Europa League iliyopigwa Jumanne mpaka Alhamisi.

Nchini England shughuli ilianza jana Ijumaa kwenye viwanja viwili wakati ambapo West Ham United wakiwa nyumbani waliendelea kuzamisha Fulham baada ya kufunga 3-1 katika mfululizo wa derby ndogo ya London.

Ushindi wa West Ham umewasogeza hadi nafasi ya 9 wakiwa kwenye kampeni ya kuhakiki wanafuzu kushiriki michuano ya Ulaya mwakani huku kipigo hicho bado kinaendelea kuiweka Fulham kwenye vita ya kujinasua kushuka daraja vita ambayo wamehusika nayo tangu mwanzo wa msimu mpaka sasa.

Kwingineko Cardiff City wakiwa nyumbani walichezea kipigo cha 5-1 kutoka Watford mchezo ambao ulihusisha timu iliyopo 10 bora na timu inayopambana kufa na kupona kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja.

Pasina shaka yoyote mchezo utakaovuta hisia za wengi kwenye ratiba ya weekend hii ni ule utakaowahusisha mahasimu wa kihistoria Manchester United na Liverpool wanaocheza pale Old Trafford Jumapili katika mchezo ambao Manchester Citu wataomba sala zao zote kuiombea Inited ishinde na kuzuia kampeni ya Liverpool kusaka ubingwa.

Jumapili hii pia tutashuhudia Manchester City na Chelsea zikicheza fainali ya kombe la Carabao, mara ya mwisho timu hizi kukutana City walishinda mabao 6-0 na Chelsea ambao wamejikuta wakipoyeza nafasi ya kutetea taji lao mbele ya Manchester United Jumatatu iliyopita kwenye kombe la FA watahitaji ushindi kama kocha Maurizio Sarri atataka kubaki kwenye klabu hii ya London.

ITALIA-SERIE A

Nchini Italia jana AC Milan ikiwa nyumbani imejipigia 3-0 Empoli na kujiongezea pointi tatu muhimu zilizoifanya waisogelee Inter Milan kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi.

Mabingwa watetetezi Juventus watakuwa kibaruani Jumapili kucheza na Bologna huku Inter Milan wakicheza na Fiorentina kwenye mchezo mkubwa wa wiki kwenye ligi hii na Napoli siku hiyohiyo Jumapili watacheza na Parma ambayo imeendelea kuwa na rekodi nzuri dhidi ya timu kubwa.

HISPANIA-LA LIGA

Nchini Hispania mabingwa wa ligi Barcelona watakuwa uwanjani leo kucheza na Sevilla huku Sevilla wakiwa wametoka kufuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Europa.

Jumapili hii itashuhudia majirani wa jiji la Madrid Atletico na Real wakiwa nyumbani na ugenini katika mfululizo wa mechi za ligi hii. Atletico atakuwa na Villarreal ambao wamekuwa na msimu mbaya huku Real wakisafiri kwenda kucheza na mbabe wao wa msimu uliopita Levante baada ya kuchezea kipigo Jumapili iliyopita mbele ya Girona.

UJERUMANI-BUNDESLIGA

Nchini Ujerumani mabingwa watetezi Bayern Munich watakuwa na mchezo dhidi ya Hertha Berlin leo huku wakifahamu fika kuwa ushindi utawafanya wawafikie vinara Burussia Dortmund.

Borussia wamekuwa kwenye kiwango duni tangu yalipoisha mapumziko ya msimu wa baridi ambapo wameshindwa kuondoka na pointi 3 kwenye mechi 5 mfululizo za michuano mitatu kwa maana ya DFB-Pokal, Bundesliga na UEFA Champions League na watajaribu kurejesha kiwango chao Jumapili watakapocheza na Bayer Liverkusen.

UFARANSA-LIGUE 1

Huko Ufaransa leo PSG watakuwa na mchezo dhidi ya Nimes huku Monaco na Olympic Lyon wakicheza Jumapili kwenye mchezo wa mwisho wa ratiba ya weekend hii kwa ratiba ya ligi ya Ufaransa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here