Home Kimataifa Mawakala maji shingoni, ada za uhamisho kulipwa na wachezaji wao

Mawakala maji shingoni, ada za uhamisho kulipwa na wachezaji wao

9671
0

Viongozi wa Ligi kuu ya soka ya Uingereza wanatarajiwa kukutana kesho alhamisi katika kuangalia jukumu la malipo kutoka vilabu kwenda kwa wachezaji.

Wachezaji wa Ligi kuu ya Uingereza huenda wakalazimika kuwalipa mawakala wao (ada ya usajili ya wakala ). Hapo awali vilabu husika vilikuwa na jukumu la kuwalipa mawakala.

Haya ni mageuzi ambayo yanatazamiwa kuwa makubwa katika soka la Uingereza.Takwimu zinasemaje?

Kwa mfano vilabu vya Premier League msimu wa 2016 vililipa kiasi cha  £174m kwa mawakala, kutoka £130m, msimu wa 2015. Manchester City ndio timu iliyolipa mawakala (£26.3m) huku Chelsea wakilipa (£25.1m) na Manchester United (£19m) kwa msimu huo.Je kuna madhara yeyote katika hili?

Huu mchakato utapelekea  wachezaji kuhitaji mishahara mikubwa.Je upande wa vilabu nao watafaidika nini?

Kumekuwa na kasumba ya vilabu kuweka dau kubwa sana kwa wachezaji ili kukidhi haja na matakwa ya mawakala. Na wakati fulani kuna mawakala wamekuwa wakichochea vilabu husika kuweka bei kibwa kwa wachezaji wao ili nao wapate fungu nono. Na huu utakuwa mwarobaini kwani itaondoa adha ya mawakala hao kuhitaji ada za kubwa za kufanikisha usajili.Msimu wa mwaka jana hali ilikuwaje?

Mwaka jana Mawakala walijikusanyia kiasi cha Pauni Milioni 220 kwa ada zao kutoka kwa vilabu nchini Uingereza na Wales. Kama mabadiliko hayo yakifanikiwa basi dili kama la Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United ambapo wakala wake Mino Raiola alipokea kiasi cha Pauni Milioni 41 kutoka vilabu vyote viwili, itakuwa jukumu la Pogba kufanya hivyo sasa, badala ya vilabu.1. Liverpool £26.8m
2. Chelsea £25.1m
3. Man City £23.5m
4. Man United £18m
5. Watford £13.4mKwahiyo masuala ya vikao ni lini?

Kikao cha Alhamisi kitaamua kama watafanya mabadiliko kadhaa ya Mapendekezo au kufanya kazi pamoja na FIFA ambao pia wanafikiria kufanya mabadiliko katika mfumo wa sasa.Je kuna Mapendekezo yeyote?

Mapendekezo hayo yapo matano….

  1. Kurejesha mitihani kwa mawakala wote kuona kama wana vigezo sahihi vya kuwa mawakala.
  2. Watahitajika kufanya biashara zao zote kupitia Benki ya UK .
  3. Watahitajika kutoka taarifa ya biashara zao za mwaka mzima kwa FA.
  4. Ada za mawakala zitakuwa zinalipwa katika kila msimu wa mkataba wa mteja wake.

Kwanini ada hiyo ilipwe kwa wakati huo?

Mfano mchezaji kasaini mkataba wa miaka mitano , basi wakala atalipwa ada yake kila msimu na sio kwa mkupuo  Lengo ni kuondoa utaratibu wa wachezaji kutaka uhamisho wa mara kwa mara .

5. Kuondoa uwakilishi pacha.

Suala la uwakilishi pacha limekaa vipi?

kwamba wakala anawakilisha Klabu na mchezaji , watalazimika kuamua kuwakilisha klabu au mchezaji na sio vyote kwa pamoja


 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here