Home Kitaifa Mbao FC marufuku kufungwa na Yanga, Simba, KMC wala Alliance

Mbao FC marufuku kufungwa na Yanga, Simba, KMC wala Alliance

7404
0

Kwenye utambulisho wa wachezaji na kuonyesha jersey mpya kwa mashabiki wa Mbao FC, club hiyo iliamua kwenda kwenye kijiwe ambacho timu hiyo ilianzishwa.

Shughuli hiyo ilifanyika maeneo ya Sabasaba Mwanza kwenye soko la kuuzia Mbao ambapo club ya Mbao FC ilianzishwa.

Mwakilishi huyo akifikisha ujumbe kwa niaba ya mashabiki alisema,“Kutokana na kuendelea kuwa na udhamini mnono na muhimu kutoka GFTrucks, sisi kama mashabiki tunawapa changamoto wachezaje wetu kwamba marufuku kufungwa na timu hizi. Kwanza Alliance ambao ni watoto wetu tunawalipia ada za shule kabisa, Simba na Yanga, pamoja na KMC. Ikishindikana waondoke na point moja lakini sio kutufunga, hili liotokee nje na ndani. Uwezo tunao na nguvu tunayo ya kutosha kutoka GFTrucks”

Ikumbukwe kwamba kocha wa zamani wa Mbao FC amehamia KMC, na Alliance ni timu inayotokea Mwanza kama Mbao FC. Mechi ya kwanza itakua kati ya Mbao FC dhidi ya Alliance.

Mbao FC ambayo chimbuko lake ni Mwanza, hadi sasa imeweza kuwa timu shindani kwenye ligi kuu ya Tanzania bara kutokana na kuwa udhamini wa uhakika kutoka GF Trucks. Mbao FC imeweza kukuza na kutoa vipaji vipya vya ndani na nje ya jiji la Mwanza.

Kampuni ya GF Trucks imetoa mchango mkubwa wa kiudhamini kuhakikisha timu hiyo ina uwezo mkubwa wa kushindana kimchezo.

GF Trucks ni wasambazaji wa magari makubwa ya kazi kama kubebea mizigo, magari ya ujenzi pamoja na vifaa vya kuchimbia madini. Ijue zaidi GF Trucks kwa kutembelea tovuti yao hapa.

http://www.gftrucks.com/

  

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here