Home Kitaifa Mbao Fc waahidi kutembeza kichapo kwa Singida United hapo kesho

Mbao Fc waahidi kutembeza kichapo kwa Singida United hapo kesho

9044
0

Na Tima Sikilo

KOCHA mkuu wa Mbao FC, Amri Saidi, amewatambia wapinzani wake Singida United kuwa ni lazima waondoke na pointi tatu za mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mbao wanatarajia kuvaana na Singida kesho katika uwanja wa Namfua uliopo mkoani humo.

Akizungumza na Mwandishi kocha huyo amesema mipango yao nikuhakikisha wanashinda kila mchezo uliopo mbele yao ili kujiweka vizuri katika msimamo wa ligi.

Amesema kikosi chao kipo vizuri na kimesha ingia mkoani Singida kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na watapambana kuhakikisha wanashinda.

“Sisi tunajiamini na tuna uamini uwezo wetu hivyo tutapambana dhidi ya wapinzani wetu Singida kuhakikisha tuna shinda,” amesema

Mchezo wao uliopita Mbao walifanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga na kuondoka na pointi tatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here