Home Kitaifa MBAO FC WAPEWA AHADI YA TSH 10,000,000 KAMA WAKIIFUNGA ALLIANCE

MBAO FC WAPEWA AHADI YA TSH 10,000,000 KAMA WAKIIFUNGA ALLIANCE

9512
0

Baada ya GFTrucks kuweka nguvu kubwa kwenye club ya MbaoFc, wadau wengine wameongezeka kui-support timu hiyo. Ikiwa ni siku chache kabla hawajacheza mechi yao ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Alliance.

Mbao FC wamepewa ahadi na Mwenyekiti wa chama cha soka chao ndani ya Wilaya ya Ilemela kwamba wakishinda mechi yao dhidi ya Alliance watapewa Tsh milioni 10. Ahadi hiyo imewasilishwa na katibu wa chama cha soka cha Ilemela kwa niamba ya mwenyekiti wake.

Siku ya Jumatano itakua mechi kali jijini Mwanza kwa timu mbili ambazo ni MbaoFc Vs AllianceFootballClub2011 ambazo zote mbili zinadhaminiwa na GFTrucks.

Mechi hii inategemewa kua ni ya ushindani mkubwa kutokana na kwamba timu zote mbili zinatokea jijini Mwanza. Hii ndio itakua official Mwanza Derby ambayo itahudhuriwa na mashabiki wengi wa jiji la Mwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here