Home Kitaifa Mbao yapokewa kifalme Mwanza

Mbao yapokewa kifalme Mwanza

3602
0

Ni mafanikio kwa Mbao kwa sababu imecheza mechi tatu bila kupoteza ndani ya dakika 90 huku ikiwa imeruhusu goli moja tu ukiachana na penati kwa ajili ya kuamua mshindi.

Imetoka sare katika mechi zake zote tatu (Mbao FC 1-1 Gor Mahia, Kariobangi Sharks 0-0 Mbao FC, Mbao FC 0-0 Simba). Gor Mahia bingwa mtetezi wa SportPesa, imefuzu hatua ya makundi ya Caf Confederation Cup.

Mbao haikufungwa na Kariobangi Sharks timu ambayo ni unbeaten kwenye ligi ya Kenya msimu huu, Kariobangi imeshiriki pia mashindano ya kombe la shirikisho msimu huu na kutolewa na Asante Kotoko wakati wa kuwania kuingia hatua ya makundi.

Wametoka suluhu na Simba kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, Simba ambayo inacheza hatua ya makundi ya #CAFChampionsLeague na bingwa wa Tanzania.

Kwa mbao ni mafanikio makubwa ingawa ilikuwa ni tournament lakini wameonesha ukakamavu wa hali ya juu hata wadhamini wao GF Trucks & Equipment ni watu wanaojivunia kuwekeza kwa Mbao FC na wanaona wapo sehemu sahihi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here