Home Kitaifa Mbwana Samatta amemjibu Mbappe

Mbwana Samatta amemjibu Mbappe

22439
0

Kinda wa Serengeti Boys Kelvin John ‘Mbappe’ kwa kinywa chake alitamka kwamba role model wake ni Mbwana Samatta, mtu ambaye anamfuatilia sana namna ya uchezaji wake na anatamani one day afikie level zake.

Salam hizo tukazifikisha kwa kwa mwenyewe Mbwana Samatta kwamba kuna dogo anatamani kuwa kama wewe na ikiwezekana avuke kwenda mbali zaidi.

Majibu ya Samatta yalikuwa hivi: “Nimefanya kazi kubwa kuwashawishi vijana wengine kucheza kwa kiwango ambacho mimi nimefika au kwenda mbali zaidi, kwa hiyo ni jambo kubwa na mimi nafurahi lakini nawausia kwamba wanaweza kuwa bora kuliko mimi si tu kufika ambako mimi nimefika lakini wanaweza kuvuka kwa hiyo waendelee kujituma nina imani watafanikiwa zaidi.”

“Niliongea nae (tulichati kwa kifupi) nilimweleza baadhi ya mambo kubwa ni juhudi halafu siku zote hakuna njia rahisi kufanikiwa. Inawezekana leo watu wakaona Samatta yupo sehemu fulani wakadhani ilikuwa rahisi alitoka akapambana akafika alipofika.”

“Hakuna njia rahisi ya mafanikio huwezi kuamka ukajikuta upo sehemu fulani, haiwezekani. Kwa hiyo ni juhudi na ajue nini anataka, kuna vitu vingi sana vinaingia kati unapokuwa unakimbiza kitu chako, asilimia kubwa vinakuwa vinakurudisha nyuma kufikia ndoto ambazo unazo.”

“Kwa hiyo aelewe hakuna njia rahisi na vikwazo vinakuwa ni vingi, akipambana anaweza kufika vilevile asisite kuomba ushauri au kujaribu kunitafuta au kumtafuta mtu mwingine yeyote ambaye anauzoefu wa soka kwa sababu sipo pekeyangu tupo wengi ambao tunaweza kumsaidia kwa njia moja au nyingine. Sio yeye tu hata kwa watoto wengine ambao wana nia na juhudi wanataka kufanikiwa wawatafute watu wenye uzoefu sio lazima wawe wanacheza nje, hapahapa Tanzania wapo wachezaji wenye uzoefu wa kuwasaidia.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here