Home Kimataifa Mchezo wa kukata na shoka Wolverhampton vs Liverpool

Mchezo wa kukata na shoka Wolverhampton vs Liverpool

3719
0

Mchezo huu utachezwa leo majira ya saa 23:00 kamili katika dimba la Molineux Stadium.


Huu utakuwa mchezo mzuri sana hasa baada ya wolves kuonesha kiwango kikubwa sana cha kuvutia msimu hasa hasa mbele ya vinaara wakubwa wa EPL.

Taarifa za timu

Wolverhampton

Wamepoteza mech 11 walizocheza siku ya Ijumaa. Huku michezo yote ikiwa ni mchezo hiyo yote ya ligi kuu England. Mara ya mwisho kushinda mchezo wa ligi kuu siku ya Ijumaa ilikuwa mwaka 1965 dhidi ya Sunderland.

Kuna uwezekano Diogo Jota akaukosa mchezo huu wa leo

Wameshinda mchezo moja kati ya michezo nane ya mwisho ya ligi kuu England, sare 2 amepoteza mara 5.

Uongozi wa Wolves umesema kuwa mchezo wa leo utakuwa maalumu kwa ajili ya nyita wao wa Zamani Bill starter ambaye aliisaidia klabu hiyo 1965 kutwaa kombe la FA. Bill Starter amepoteza uhai wake jumatatu ya wiki hii

Mara ya mwisho kumfunga Liverpool, ilikuwa mwaka 2010 bao 1-0 katika uwanja wa Anfield chini ya kocha Mick McCarthy.


Liverpool

Liverpool baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya United leo watashuka uwanjan wakiwa na morali ya hali ya juu.

Katika michezo mitano ya mwisho dhidi ya Wolverhampton, katika uwanja wa Molineux ameshinda mara 2 na sare 3 pia hawajaruhusu bao katika michezo hiyo.

Katika michezo 18 ya ligi kuu England ajapoteza mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1990 walishinda michezo 23.

Nyota wa mchezo
Salah, amehusika katika upatikanaji wa mabao 10 katika michezo 8 ya ligi kuu dhidi ya timu zilizopanda daraja mabao 5 na assist 5.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here