Home Ligi EPL Mechi 3 za mwanzo kwa Jose Mourinho kwa misimu 9 zilikuwa hivi…..,...

Mechi 3 za mwanzo kwa Jose Mourinho kwa misimu 9 zilikuwa hivi….., abaki aondoke?

8526
0

Tangu baada ya kipigo kutoka kwa Tottenham Hotspur siku ya Jumatatu, kocha Jose Mourinho amekua akiandamwa sana karibia kila pande ya dunia.

Hii inawezekana kuwa ni mkosi wa Mourinho katika msimu wa tatu kama ambavyo ilikuwa kote alikotoka. Leo sii vibaya tukatazama mechi zake 3 za mwanzo kwa misimu 9 huko atokako kabla ya United kufanya maamuzi.

2010/2011

19/08/2010 (Mallorca 0 Real Madrid 0)

11/09/2010 (Real Madrid 1 Osasuna 0)

18/09/2010 (Real Sociedad 1 Real Madrid 2)

Jumla ya alama 7.

2011/2012

28/08/2011 (Real Zaragoza 0 Real Madrid 6).

10/09/2011 (Real Madrid 4 Getafe 2).

18/09/2011 (Levante 1 Real Madrid 0)

Jumla ya Alama 6.

2012/2013

19/08/2012 (Real Madrid 1 Valencia 1).

26/08/2012 (Getafe 2 Real Madrid 1).

2/09/2012 (Real Madrid 3 Granada 0).

Jumla ya alama 7.

Katika misimu hii mitatu Mourinho akafanikiwa kuwapa Real Madrid ala Liga 2011/2012, Copa Del Rey 2010/2011 na Super Copa mwaka 2012.

Mwaka 2013 tarehe 22 Mourinho akasaini mkataba mpya Real Madrid ulikuwa ukimuweka hadi 2016 lakini tarehe 23 May 2013 Real Madrid wakatangaza kwamba Mourinho hatakuwa nao kwa msimu unaokuja wa ligi.

Baada ya Mourinho kuondoka Real Madrid, ilipofika tarehe 3 mwezi wa sita mwaka 2013 ikathibitishwa kwamba Mou anarejea tena The Blues nako hali ikawa hivi.

2013/2014

18/08/2013 (Chelsea 2 Hull City 0).

21/08/2013 (Chelsea 2 Aston Villa 1)

26/08/2013 (Man United 0 Chelsea 0)

Jumla ya alama 6.

2014/2015

18/08/2014 (Burnley 1 Chelsea 3).

23/08/2014 (Chelsea 2 Leicester 0).

30/08/2014 (Everton 3 Chelsea 6)

Jumla ya alama 9

2014/2015 Mourinho akawapa Chelsea kikombe cha EPL bila.kusahau kikombe cha ligi msimu wa 2014/2015.

2015/2016

08/08/2015 (Chelsea 2 Swansea 2)

16/08/2015 (Man City 3 Chelsea 0)

23/08/2015 (Chelsea 3 West Bromich 2)

Jumla ya alama 4.

Msimu wa 2015/2016 mambo yalimchachia Jose Mourinho kwani katika mechi 16 za mwanzo alipigwa mara 9, Chelsea ikawa iko nafasi ya 16 na Roman Abromovich hakumvumilia akamtimua.

Tarehe 27 May baada ya Mourinho kutimuliwa Chelsea, United wakamtangaza kuwa mwalimu wao mpya.

14/08/2016 (Man United 3 Fc Bournemouth 1

19/08/2016 (Man United 2 Southampton 0)

27/08/2016 (Man United 1 Hull City 0).

Jumla ya alama 9.

2017/2018

13/08/2016 (West Ham 0 Man United 4).

19/08/2017 (Man United 4 Swansea 0).

26/08/2017 (Man United 2 Leicester 0).

Jumla ya alama 9.

2018/2019

(Man United 2 Leicester City 1)

(Brighton 3 Man United 1)

(Man United 0 Tottenham 3).

Jumla ya alama 3.

Hadi sasa tangu ajiunge na United, Jose Mourinho ameshawapa kombe la EFL msimu wa 2016/2017, wakashinda ngao ya hisani 2016, na kikombe cha Europa 2016/2017. Apewe muda au aondoke?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here