Home Kimataifa Messi amwagia Ronaldo sifa, asema Atletico imemchania mkeka

Messi amwagia Ronaldo sifa, asema Atletico imemchania mkeka

3296
0

Kumekuwa na picha inasambaa mtandaoni ikionesha mawasiliano ya whatsapp kati ya Evra na Ronaldo. Katika mazungumzo hayo Evra anamsihi Ronaldo kuhakikisha kuwa anawatoa Atletico.

“Bro kila unaposhindwa kufunga au Juve ikifungwa nakosa amani mtaani. Kila mtu ananizomea. Nakuaminia kaka” Evra

Ronaldo akamjibu akamwambia “Usijali bro”

Sasa baada ya Ronaldo kutimiza ahadi ya Evra, Messi amejitokeza na kumwagia sifa kedekede mchezaji huyu bora kabisa kuwahi kutokea katika michuano ya UEFA kwa kudai kuwa alifanya maajabu.

“Nilitegemea sana Atletico wataleta ubishi kutokana na uimara wao wa kuzuia. Lakini Ronaldo alifanya miujiza.”

“Sikutarajia kama Juventus wangepita, hongera kwa Ronaldo kwa kufunga magoli mawili” Messi.

#Class #Legend #MessiRonaldo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here