Home Kitaifa Mgomo mwingine Yanga

Mgomo mwingine Yanga

32468
0

Na Tima Sikilo

NYOTA watano watimu ya Yanga wapo kwenye hati-hati ya kuukosa mchezo wao wa marudiano dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda unaotarajiwa kuchezwa Jumatano ijayo nchini Rwanda.

Mchezo wao wa kwanza wa michuano hiyo ulichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na kumalizika kwa suluhu.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo, zinasema kuna wachezaji watano wakubwa ambao wameshindwa kufika mazoezini wakidai hadi wakamilishiwe stahiki zao.

Inaelezwa kuwa kocha wa Yanga hafurahishwi na kitendo hicho kwani mwisho wa siku wachezaji wanaweza kujiunga na timu kuelekea nchini Rwanda wakiwa hawana mazoezi.

“Wachezaji ambao hawajafika mazoezini ni watano lakini siwezi kuwataja majina mtawaona wenyewe siku ya mechi, hii si nzuri sana kwani inaweza kuleta athari pale watakapokubali kwenda Rwanda huku wakiwa hawana mazoezi,” kimeeleza chanzo hicho.

Amesema kutofika mazoezi wakati wanajua fika wanatakiwa kuwa sehemu ya  mchezo sio jambo zuri na wanapaswa kufahamu thamani yao katika kikosi hicho.

Wengine ambao hawatakuwepo katika mchezo huo ni Mrisho Ngasa, golikipa Mkongo Klaus Kindoki na Fei Toto ambao  usajili wao haukukamilika Caf.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here