Home Kimataifa Mke wa Icardi ataka Tsh bilioni 30, Madrid yamwekea Koulibaly Tsh bilioni...

Mke wa Icardi ataka Tsh bilioni 30, Madrid yamwekea Koulibaly Tsh bilioni 270

6089
0

Inasemekana Chelsea wapo mbioni kuvunja mkataba wa mkopo wa Michy Batshuayi kutoka klabu ya Valencia. Michy ameitumikia Valencia mwezi mmoja tu na klabu ya Chelsea ipo mbioni kumrudisha mapema darajani.


Klabu ya Real Madrid ipo tayari kutoa dau la £90M sawa Tsh Bilioni 270 ili kumnasa Kalidou Koulibaly anayewaniwa na klabu ya Man United.


Klabu ya Arsenal ipo mbioni kunasa huduma za kiungo kutoka Porto Hector Herrera ili kuziba pengo la Aaron Ramsey. Herrera mwenye miaka 28 mkataba wake unaisha mwezi june.

Unai pia anawania kuoata huduma za winga wa zamani wa Atletico Yannick Carrasco. Carrasco kwa yupo China anakichafua kunako klabu ya Dalian Yifang


Klabu ya Juventus ipo tayari kumuongezea Massimalano Allegri mshahara mpaka kufikia £9M. Allegri anawindwa kwa karibu sana klabu ya Real na Man united


Mauro Icardi amepewa ofa ya mkataba wa £7M kwa mwaka lakini wake ambaye ni mke wake Wanda amesema mshahara huo ni mdogo anataka £9M sawa na Tsh Bilioni 27. Icardi mwenye miaka 25 anawindwa sana klabu za Madrid na Chelsea kwa dau la £100


Jarida la Mundo Deportivo limesema kinda wa Ajax anayewaniwa na miamba mbalimbali wa Ulaya Frenkie de Jong amekubali kusaini mkataba na vigogo wa Hispania Barcelona.

Ikumbukwe pia kiungo wa PSG Adrien Rabiot nae amekubaliana na Barcelona kusaini katika klabu hiyo.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here