Home Kitaifa Mkuu wa wilaya aipeleka Simba robo fainali CAF

Mkuu wa wilaya aipeleka Simba robo fainali CAF

7468
0

Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba Adam Mgoyi amesema Simba nj moja ya vilabu vitakavyofuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Mgoyi amesema kundi ilipo Simba ni gumu lakini imeonesha nia ya kufanya vizuri katika hatua zote toka inaanza mechi za hatua za awali za ligi ya mabingwa Afrika.
.
“Simba ni timu nzuri kwa kiwango cha mpira wa Tanzania nadhani ni timu bora na haya yaliyotokea hayajatokea kwa bahati mbaya kwa sababu viongozi walijipanga na wakaweka ahadi ya kufika hatua ya makundi kwa hiyo hawajaingia kwa bahati mbaya.”
.
“Aina ya timu ambazo zipo kwenye makundi lazima ziwe bora kwa sababu timu 16 Afrika nzima zilizoingia hakuna timu dhaifu kwa sababu hata sisi tumeingia kwa kuitoa timu bora Nkana kwa hiyo tunaenda kushindana na timu zenye uwezo kama sisi, kitakachotokea ni matokeo ya mpira.”
.
“Kwa uwezo wa mwalimu tuliyenae na kwa uwezo wa wachezaji wetu naimani tutaingia hatua ya robo fainali.”

Mgoyi amesema ukichunguza timu zilizofuzu hatua ya makundi utaona timu nyingi zimewahi kuwa mabingwa wa mashindano haya kama sio klabu bingwa basi ni kombe la shirikisho kwa hiyo timu ambazo zimepangwa kundi moja na Simba ni sawa na za makundi mengine.

Anasema Simba waliwahi kuitoa Zamalek pamoja na kuzifunga timu nyingine za kiarabu kwa hiyo hakuna shaka kikubwa ni kocha kuwaandaa wachezaji na wao wawe tayari kupambana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here