Home Uncategorized Mmh kwa takwimu hizi Watford wanaamini wanaweza kubeba EPL msimu huu

Mmh kwa takwimu hizi Watford wanaamini wanaweza kubeba EPL msimu huu

9837
0

Kati ya vitu vya kusisimua sana vinavyoendelea EPL ni namna ambavyo Watford wamegoma kuondoka Top 4, hadi sasa wako nafasi ya 3 na alama 12, hawajapoteza mechi hata moja.

Nikurudishe nyuma msimu wa 2014/2015, Leicester City walimaliza msimu huu wa ligi wakiwa na alama 41 huku nafasi katika ligi wakimaliza wakiwa wa 14.

Msimu ule Leicester walionekana wanashuka daraja, michezo 11 wakashinda, wakapata suluhu 8 na vipigo 19 lakini mungu si Athumani, wakafanikiwa kubaki kwenye ligi.

Msimu uliofuata (2015/2016) hakuna aliyetarajia, kocha Claudio Ranieri akawapa Leicester City kombe tena mbele ya timu vigogo za EPL.

Msimu uliopita Watford wakapokea vipigo 19, suluhu 8 na ushindi mara 11 huku wakimaliza nafasi ya 14 kama vile vile ambavyo Leicester City walifanya 2014/2015.

Na msimu huu Javi Gracia na vijana wake wako nafasi ya tatu hadi sasa na hakuna dalili ya wao kuondoka hapo juu hivi karibuni, Its happening😂

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here