Home Entertainment Mo Salah awaacha mbali Davido, Wiz Kid na Didier Drogba

Mo Salah awaacha mbali Davido, Wiz Kid na Didier Drogba

10751
0

Baada ya hapo jana kuona kwamba Simba ndio klabu yenye followers wengi Afrika Mashariki na Kusini, kuna mtu aliniuliza kwenye mziki na soka ni nani ana wafuasi wengi Instagram?

Niliamua kuperuzi mtandaoni ili kujua ni nani ambaye anaongoza kwa wingi wa followers Instagram katika muziki na soka na hii hapa nikaipata kama 5 bora Afrika.

5.Wiz Kid. Hit maker wa ngoma inayosumbua zaidi Africa Socco anashika nafasi ya 5 katika mastaa wa Kiafrika ambao wana followers wengi akiwa na followers 5.8m.

4.Didier Drogba. Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea lakini vilevile timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba ndiye ambaye yuko juu ya Wiz Kid ambapo katika mtandao ana followers 6.5m.

3.Davido. Msanii bora zaidi Afrika kwa sasa ambaye anatamba na ngoma kama vile If na Fia huku kwa sasa akowa habari kubwa baada ya kununua ndege binafsi ana followers 7m.

2.Pierre Aubameyang. Mchezaji wa Arsenal ambaye hapo juzi alitimiza ndoto yake ya kutembea katika uwanja wa WWE ndio anashikilia nafasi ya pili akiwa na followers 7.4m.

1.Mohamed Salah. Salah ndio mfalme kwa bara la Afrika katika mtandao wa Instagram, mchezaji huyo bora wa Liverpool na Epl kwa ujumla ana followers 19.6m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here