Home Kimataifa Mourinho afanya mabadiliko kwenye kikosi alichosafiri nacho

Mourinho afanya mabadiliko kwenye kikosi alichosafiri nacho

13166
0

 

Manchester United imesafiri na baadhi ya wachezaji wake kwenda kufuana na Burnley


United wanatarajia kwenda Turf Moor huku wakiwa na rekodi mbaya ya kupoteza michezo miwili ya hapo awali.

Eric Bailly, Anthony Martial, Juan Mata na Sergio Romero wamerudishwa tena kikosini

Bailly aliachwa kwenye mchezo dhidi ya Spurs lakini nae amejiunga na wachezaji wenzake kwenye hotelo ya Lowry, pia kuna ongezeko la Martial na Mata, ambao waliondolewa kwenye kikosi dhidi ya Spurs.

Taarifa zinadai kuwa mchezo wa leo kwa Mourinho huenda ukaamua hatma yake.

Romero na Diogo Dalot wamerudi kutoka majeruhi baada ya kucheza kwenye mchezo dhidi ya Stoke ndani ya Old Trafford. Phil Jones atakuws nje kutokana na majeraha na Rojo bado hajawa sawa kucheza.

Wachezaji ambao hawajaonekana na wenzao hotelini ni Andreas Pereira na Matteo Darmian.


 Kikosi

David de Gea, Sergio Romero, Lee Grant, Antonio Valencia, Eric Bailly, Chris Smalling, Victor Lindelof, Luke Shaw, Ashley Young, Scott McTominay, Marouane Fellaini, Ander Herrera, Nemanja Matic, Fred, Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Marcus Rashford, Romelu Lukaku, Anthony Martial, Alexis Sanchez

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here