Home Kimataifa Mourinho afungwa mwaka mmoja

Mourinho afungwa mwaka mmoja

11729
0

Meneja wa Man United Jose Mourinho amefanya makubaliano na mamlaka ya kodi nchini humo kuhusu sakata lake la ukwepaji kodi. Mamlaka hiyo imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa hilo la ukwepaji kodi nchini Hispania.


Waendesha mashitaka wa Hispania walimpeleka Josembele ya bodi hiyo kwa madai kuwa kocha huyo alikwepa kulipa kodi ya pauni milioni 2.9 ambayo yalitokana na mapato yake ya haki za picha mwaka 2011 na 2012, wakati huo akihudumu kama kocha wa Real Madrid.

Jose aliiridhia makosa hayo na kukubali kulipa  faini ya pauni milioni 1.8 ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya kodi ambayo hakulipa hapo awali.


Mreno huyu mwenye asili ya majigambo hatokwenda kuhudumu kifungo chake magereza kutokana na sheria ambayo zinasema kuwa hukumu yoyote chini ya miaka miwili kwa mtu aliyekutwa na hatia kwa mara kwanza haimlazimu kwenda jela kama mahakama itaridhia na ukubwa wa kosa lake.


Hata hivyo uongozi wa Manchester United waliofika mahakamani hawakusema lolote juu ya sakata hilo.


Shirika la ukusanyaji mapato la hispania siku za hivi karibuni limekuwa na hulka ya kufuatilia sana dokumenti za mastaa wa soka kuhusiana na janja janja yao ya ukwepaji kodi. Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Javier Mascherano na Alexis Sanchez ni moja kati ya wachezaji waliokutwa na tuhuma hizo.


 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here