Home Uncategorized Mourinho aitwa na UEFA kujadili sheria ya mabao ya ugenini

Mourinho aitwa na UEFA kujadili sheria ya mabao ya ugenini

10833
0

Makocha wakubwa duniani akiwemo José Mourinho wameitwa kwenye kikao cha Uefa cha kujadili mustakabali wa magoli ya ugenini. Moja ya hoja nyingine kubwa ni kujadili uwezekano wa madirisha ya usajili ya nchi wanachama kufungwa kwa wakati mmoja.

Naibu katibu mkuuwa uefa bwana  Giorgio Marchetti  amethibitisha kuwa kutakuwepo na kikao hicho na wanatarajia kuangalia ukakasi wa mabao ya ugenini na ya nyumbani kama kweli kuna uwezekano wa kuondoa utaratibu huo hasa kwenye hatua za mtoano.

Makocha wengine walioalikwa ni Massimiliano Allegri (Juventus), Carlo Ancelotti (Napoli), Unai Emery (Arsenal), Paulo Fonseca (Shakhtar Donetsk), Julen Lopetegui (Real Madrid), Thomas Tuchel (Paris Saint-Germain) na kucha wa zamani wa Arsenal  Arsène Wenger.

“Makocha wengi wanaamini kufunga mabao ugenini sio kazi ngumu kama ilivyokuwa hapo awali, hivyo kigezo bicho kinaoaswa kichunguzwe tena upya” Marchetti

Giorgio Marchetti akiwa na Thomas Tuchel,
Sheria hii ilitambuloshwa katika michuano ya  European Cup Winners’ Cup mwaka 1965 kama njia mbadala ya kuondoa urushaji wa sarafu kama njia ya kuamua mshindi.

Makocha pia wanataka dirisha la usajili lifungwe na kufungulia siku moja ili kuwepo na usawa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here