Home Ligi EPL Mourinho akiona kunguru wamepungua mtaani, nyama za kuku ni nyingi na zimeshuka...

Mourinho akiona kunguru wamepungua mtaani, nyama za kuku ni nyingi na zimeshuka bei awe mwelewa

16987
0

Bila shaka hakuna tena haja ya kumuongelea Mourinho kwa namna nyingine zaidi ya kusema “Ele precisa descansar” (Kireno) Yaani anahitaji kupumzika kidogo. Arudi tena mpaka kule mjini Setubol au aende Marekani akapumzishe kichwa kisha aruddi tena.

Kwa sababu kwanza yupo sehemu sahihi kabisa. Pili yupo timu kubwa. Tatu ana kila kitu nyuma yake. Nne ana jeuri ya historia ya klabu anayofundisha, ubabe wa kifedha na wachezaji lukuki. Je kwanini an

Yule mpinzani wake mkubwa Pep.
yeye anatamba tu. Waswahili husema cha kipofu, kimo mkononi mwake, Pep anatumia njia zile zile za Mou za kutumia fedha nyingi kumuadhibu. Kweli nimeamini fitna, ngozi ya tembo.

Mourinho imefika mahali analalamika timu nyingine zinamwaga fedha (Klopp)

Mourinho anayumba kama tanga linalopelekwa na kimbunga. Siku hizi ukifuatila mikutano yake na waandishi wa habari zinahuzusha sana kama wewe ni shabiki wa United. Kwanza yeye mwenyewe hana matumaini na klabu yake. Amekuwa mwepesi hasira w
za hovyo hovyo. Muda mwingi anatumia sana kulalama kuhusiana na bodi. Inaonesha picha wazi kuwa hata bodi haimuamini tena. Bodi imesitisha kumpa fedha za usajili. Kwanini? Kwa sababu hata wale wachezaji alio wanunua mwenyewe hawahitaji sana (Mkhitaryan). Wengine wanacheza chini ya kiwango (Sanchez).

Kabla ya ligi kuanza alisema kuwa msimu huu utakuwa mgumu sana kwa United. tehe tehe mwangua madafu, daima huishi kwa hofu.

Leo wamepigwa na Brighton goli tatu. Amesema hata kumlaumu mchezani yeyote. Sawa najua huu ni unafiki tu. Kwani nani hakuona mabeki wake walivyokuwa wanatetemeka kama wanywa gongo? Amekuwa na malalamiko kuhus safu ya ulinzi. Na atajificha kwenye kivuli kwamba niliomba timu isajili mabeki na wamekataa.

Kila siku anasema shida ni mabeki, lakini nani alisema kamba inapandi bila mti? Shida sio mabeki ila anapaswa ajue mgeni hapewi kiporo. Mfumo wake wa kizamani anataka kuwalazimishia vijana wa kileo. Kwani hao washambuliaji wake mbona hawafanyi maajabu ili tusema mabeki ndio waliozingua? Timu kama Liverpool zilikuwa na mabeki wazito lakini washambuliaji wake walikuwa wanafunga. Tunadanganyana tu.

Hata Mwalimu Nyerere alikuwa shujaa wetu. Mkubwa sana. Kila mtu alimuheshimu. Sisi watanzania wengine na wote tukamweka tabaka la juu tukaamini kuwa yeye ndiye mtawala wetu. Hakuna aliyejinua kumpinga wala kujaribu kumdhibiti. Sawa na Mourinho tu. Hakuna kocha aliyemsumbua tena kwa mafanikio yake. Hata Ferguson alijua wazi Jose ni mtu mbaya. Lakini Mwalimu Nyerere ilifika mahali akaona mbinu zake zinakwenda kinyume na matakwa ya dunia.

Hakutaka kubishana na uhalisia. Kila chombo na wimbile. Hakutaka kuongozwa na dhana za kimajinuni. Akabwanga manyanga akasema NANG’ATUKA. Unadhani mwalimu alipachoka ikulu? Unadhani hakupenda kuendelea kuitwa Raisi? Hapana! Kuna wakati duniani inakwenda tofauti na ulimwengu wako wa ndani.

Gaddafi na ubabe wake wote aliishia pabaya. Labda Mourinho kama anataka kushushiwa taulo lake na ilhali hataki kuchutama basi akubali kumwaga radhi. Twende mbele turudi, Mourinho ni kocha mzuri na mbovu kuwahi kumuona. Ana mafanikio lukuki lakini mshale wa saa kwake umesimama. Anataka kutupeleka zama za mawe. Soka lake limekwenda na wakati lakini anataka kufa na tai shingoni. Sawa kama anataka kuendelea kupambana mpaka mwisho ajue tu kwamba ukipanda mvule, matone yake uyavumilie.

Mourinho amenizidi mengi lakini soka lake la maji taka kila mtu analiona labda vipofu tu ndo wakisikia mafanikio ya Mou hawawezi kukubaliana na mimi kuwa Mou anapaswa kupumzika. Sio kila palipo tuna, pamenona na hili lipo wazi kwa Mourinho kwamba rekodi yake ni nzuri lakini kwa sasa amekuwa mnywa maji kwa mkono na kiu yake ipale pale. Yaani matokeo yake ni kududnduliza tu. Anashinda kimazabe tu.

Akajifue upya arudi tena na mbinu nyingine. Na akubaliane na hali kuwa mshale wa saa haurudi nyuma asilazimishe mihogo kuwa baga.

Abadilike kuanzia namna ya ufundishaji na namna ya kuishi na wachezaji. Hajafeli ufundishaji tu amefeli hata namna ya kuishi na wachezaji. Wachezaji wa zamani walikuwa tayari kutumikishwa kama punda. Hilo soka siku hizi hakipo Mbappe ana miaka 19 ana lipwa zaidi ya laki mbili kwa wiki je ukimtolea maneno makali na kumpelekesha atakuelewa kweli??

Akina Martial wanacheza kama wapo magereza. Yaani Martial akikosea kidogo tu lawama zote kwake. Yale yale ya kila agombanae na mchawi, akiumwa huhisi amerogwa.

Watu wanadhani wachezaji wa Man U ni wabovu, hapanaa, Moruinho anatumia mbinu za kuvuruga mawazo ya wengi. Anawalaumu wachezaji kiasi cha kuwapotezea mudi zao. Si unajua mjanja anapoudhika, mjinga husuuzika. Hawana furaha na wala hawana amani. Amefeli Chelsea na amefeli hapa Ma United tena nina imani huu ni msimu mwingine atatoka kapa. Aibu ni kujikwaa kisiki kimoja mara mbili lakini apumzike tu. Awe mwelewa dunia imebadilika.

Kichwa habari kinahusu nini? Mourinho anataka kuku. Nikimaanisha anahitaji wachezaji wanaoendana na mfumo wake. Kile anachokihitaji yeye bodi ya Man United imeshtuka dunia imebadilika. Nikimaanisha watu wanauza kunguru badala ya kuku. Mourinho anashindwa kutofautisha kati ya kunguru na kuku. Yaani anashindwa kutofautisha soka lake la zamani na soka la sasa. Anakoenda anawalazimishia Man United nyama ya kunguru badala ya kuku..

Ni Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here