Home Kimataifa Mourinho alikumbana na mengi

Mourinho alikumbana na mengi

4839
0

Katika ulimwengu wa soka ukitaja jina la kocha Jose Mourinho, sio ngeni kutokana na umarufu wake pamoja na mataji aliyotwaa akiwa katika klabu mbali mbali Barani Ulaya.

Jose amewahi kuzifundisha timu zifuatazo kama Inter Milan, Chelsea, Fc Porto, Real Madrid, na Manchester United, kote amefanikiwa kutwaa mataji katika karne yake ya soka ametwaa mataji 25.
Jose Mourinho, msimu huu ameshindwa kuiongoza Utd kufanya vizuri Katika ligi kuu England, ukimuuliza sababu kubwa atakwambia timu aijafanya sawa linawezekana au kwa mtazamo wake? Lakini ukiangalia Manchester United, ya msimu huu na msimu uliopita aina utofauti sana karibia wachezaji ni wale wale ukimtoa Fred, na Dalot, msimu uliopita walimaliza nafasi ya pili huku wakiruhusu mabao 28 msimu mzima.

Msimu huu zikiwa zimechezeka michezo 17 wameruhusu mabao 29 pengine mbinu za Jose Mourinho, zinawafanya wachezaji kushindwa kucheza wamekuwa wanacheza kukamilisha ratiba.Kiukwel Jose, aliishiwa mbinu toka mda lakini kuna baadhi ya watu walishindwa kuelewa au kuamini huku wakidhani bodi inamuangusha ukitoa bodi ya timu pia wachezaji wengi wa United, ni wabunifu kwa maana ya uwezo mkubwa uwanjani.

Wachezaji kama Fred, Mata, Pogba, Sanchez, wote wana uwezo mkubwa wa kukupa kitu muhimu lakini Jose, ameshindwa kuweka muunganiko wa timu nzima kwa sababu mfumo wa kujilinda umeshindwa kuwapa wachezaji hao faida.

Mpira wa sasahivi ukiangalia timu nyingi zinazuia kwa kukaba na kwa maana sio kukaa nyuma mbele ya goli hapana? bali wanajilinda kukaa na mpira me binafsi niliamini mbinu za Jose, zilishafeli toka mda.

Bali aliishia kujibizana ovyo au kuwajibu ovyo waandishi wa habari wachezaji ambao walikuwa wanaonekana wabovu naamini Michael Carrick atawabadilisha kwa maana ya kucheza soka la kushambulia.

Ujumbe kutoka kwa Aziz Mtambo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here