Home Ligi EPL Mourinho inatosha sasa

Mourinho inatosha sasa

5358
0

Hivi Mourinho alijua mashabiki wa United walikuwa kifua wazi kwenye mabanda umiza wakishindilia kwa kauli yao ile ya “MOU NDIO MASTA WA BIG MECHI, HUYU LIVER TUNAMLA HAPA HAPA KWAO”??? mwisho mashabiki wameondoka kwa fedheha huku kila mmoja akiwana maswali mengi kichwani.

Sisi wachambuzi tumemlinda sana Mou kwa utetezi kuwa bodi inamsumbia Mou. Lakini ukiangalia kwa makini Man U ishu sio utendaji ila fomula za Mou ni nzuri lakini haziwafai wachezaji wake.

United ina wachezaji wengi wabunifu
Juana Mata, Fred, Sanchez Martial na Pogba. Wachezaji hawa wote wana uzoefu mkubwa na ni mafundi kuzidi hata safu ya kiungo la Liverpool. Nani asiyejua uwezo wa Sanchez? Pogba kuna haja ya kuuliza? Matic nae je? Kwani kuna mtu hajui kama Mata alikuwa mchezaji bora wa Chelsea misimu miwili mfululizo? Martial ndiye mfungaji bora wa United kwa sasa lakini leo alikuwa benchi?

Kuna baadhi ya mechi huhitaji kuangalia form ya mchezaji ila uzoefu. Mechi ngumu mara nyingi zinahitaji uzoefu na uwezo. Inaoensha uwezo wa Mou una kikomo. Yaani kama wachezaji alio nao hawafiti kwenye mfumo wake, basi hawezi kubadilika kwendana na mahitaji ya kikosi chake. Kuna wakati mwalimu unapaswa kubadilika kwendana na idadi ya wachezaji ulio nao au mfumo mzima wa ligi.

Pep alipogundua EPL ni ngumu hakuona aibu kubadilika kwendana na mfumo wa ligi akasajili mabeki kibao kwa gharama nyingi sana.

Baily, Lindleof, Valencia na Ashley Young sio wazuri sana lakini pia sio wabovu sana. Matic inaonekana amechoka, Mou analazimisha kwa sababu tu ananguvu za ukabaji, lakini kwani nani haoni kama Matic anakaba kwa macho?

“Mbinu zake zilishafeli ila watu hawataki kuamini. Timu haijulikani inacheza nini pasi wanabahatisha halafu hakuna muunganiko, yaani kila mtu anakimbia kimbia tu uwanjani. Siangalii tena man utd mpaka morinho afukuzwe” Issa Masoud CPA.

Kila shabiki wa United analalamika kuwa United ni mbovu kimfumo. Walio wengi wandhani Lukaku mbovu. Sio kweli Lukaku sio mbovu, ila Mou anamchoresha Lukaku. Lukaku ni namba 9 kiasilia.

Ni mchezaji ambaye kimsingi tunamwita free role yaani anakuwa huru kukaba au kukimbizana na viungo. Lukaku anatesekana sana. Anahaha sana muda mwingi anakuwa amekosa nguvu na anakuwa hoi. Yaani ukiwaangalia wachezaji wengi wa United wamekata tamaa. Wanacheza tu ili kesi isianze kwao.

Timu imeruhusu mabao mengi mno mzunguko wa kwanza. Nimejaribu kuangalia takwimu za United kuruhusu mabao machache kwa msimu

2007/08: 22 [ Mechi 38]
2008/09: 24 [ Mechi 38]
2003/04: 26 [ Mechi 38]
2006/06: 27 [ Mechi 38]
2008/09: 28 [ Mechi 38]
2017/18: 28 [ Mechi 38]

Msimu huu wa 2018/19 Tayari United imekwisha ruhusu mabao 29 huku ikifunga mabao 29. Ni rekodi mbaya ya ulinzi.

Msimu ambao United ilifungwa magoli mengi

1930/31: 115 [Mechi 42]
1929/30: 88 [Mechi 42]
1892/92: 85 [Mechi 30]
1960/60: 81 [Mechi 42]
1927/28: 80 [Mechi 42]
1959/60: 80 [Mechi 42]

DODOSO
Mara ya mwisho United kuwa na rekodi mbovu kama hii ni mwaka 1989/1990 ambapo United ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya 13 huku ikifunga magoli 46 na kufungwa 47.

United 2018 vs United 1989

Magoli ya kufunga
Man Utd 2018: 29
Man utd 1989: 28

Magoli ya kufungwa
Man Utd 2018: 29
Man Utd 1989: 24

Ushindi
2018: Ushindi mechi 7
1989: Ushindi mechi 6

Ukijaribu kuangalia ni Man United ile ile iliyomtesa Ferguson.

MAN UNITED’S TOP 5 YA MISHAHARA

1. Alexis Sanchez – £450,000

2. Paul Pogba – £260,000

3. Romelu Lukaku – £220,000

4. David de Gea – £200,000

5. Juan Mata – £145,000

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here