Home Kimataifa Mourinho maji shingoni, akiri msimu ujao ni mgumu kwao

Mourinho maji shingoni, akiri msimu ujao ni mgumu kwao

10396
0

‘WOODWARD ANAJUA KILA KITU NINACHOHITAJI. NIWAAMBIENI TU KWAMBA MSIMU HUU UTAKUWA MGUMU SANA’

Jose Mourinho kocha mkuu wa Manchester United amesema kuwa msimu huu utakuwa mgumu kwake na sababu kubwa ni mkurugenzi wa klabu hiyo.

Mourimho amesema hawaonei donge Liverpool kwa uwekezaji mkubwa lakini pia timu yake ilihitaji mabadiliko makubwa sana.

Jose Mourinho amesema the Red Devils wajiandae kisaikolojia msimu ujao wala wasitegemee makubwa.

“Ndio msimu utakuwa mgumu sana kama hatutapata majina maoya kabla ya dirisha kufungwa” Mourinho

Mabingwa Man City ambao walimaliza ligi kwa tofaut ya alama 19 dhidi ya United msimu uliopita wamemsajili Riyad Mahrez kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku Liverpool ikiwanasa Fabinho, Naby Keita, Xherdan Shaqiri na Alisson.

Lakini Mourinho amemnasa Fred na kinda wa kireno Diogo Dalot, huku Lee Grant akijiunga kwa usajili huru.
Mourinho anamsaka mlinzi wa Leicester City Harry Maguire na mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld. Kuna taarifa pia zinadaia wanahitaji huduma za Yerry Mina ingawa jitihada zao zimegonga mwamba.

Akiongea na Televisheni ya Man United (MUTV,) Mourinho amesema: “bosi wangu [Ed Woodward] kwa muda mrefu anafahamu ninachokihitaji.

“Najua amejaribu kwa kiasi chake kunisaidia, lakini bado nahitaji mengi yafanyike, bado nasubiri kuona mwisho wake.”

“kuna vilabu vinashindana na sisi na wapo vizuri, Chelsea, Tottenham, Manchester City…na usajili mkubwa wa Liverpool, ambao wananunua kila kitu na kila mtu.

“kwa hiyo tusipokuwa makini mambo yatakwenda mrama kwetu.”

Manchester United watacheza mchezo wao wa kwanza na Leicester City on agosti 10 pale Old Trafford.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here