Home Kimataifa MRI ni tiba kwa kansa inayoteketeza soka la Afrika

MRI ni tiba kwa kansa inayoteketeza soka la Afrika

10014
0

Udanganyifu wa umri bado ni changamoto kubwa sana kwa soka la Afrika.


Hivi majuzi shirikisho la soka la Afrika CAF limekumbana na sakata la ulaghai wa umri kwa mashindano ya vijana wadogo. Mwezi Agust, wachezaji watatu wa Kenya waliondoshwa kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya   CECAFA U17 yaliyofanyika hapa Tanzania baada ya wachezaji kufeli vipimo vya MRI.

Wiki hii timu ya taifa ya  Benin ya U17 waliondoshwa kwenye kushiriki michuano ya WAFU-B U17 baada ya nusu ya wachezaji wake kufeli vipimo vya MRI. Nchi za Niger, Burkina Faso, Togo, Nigeria na Cote d’Ivoire walikutwa na mchezaji mmoja mmoja waliozidisha umri na kurudishwa makwao.

Matumizi ya ulazima ya Magnetic resonance imaging (MRI) ambacho ni kipimo cha kupima uwezo wa mtu mifupa na maeneo muhimu ya mwili wa binadamu kama ubongo, ili kubashiri umri wa mtu kilitambulishwa na FIFA mwaka 2009 katika michuano yote ya FIFA U17 World Cup. MRI kinaweza kutoa majibu sahihi kwa 99% kwa mtoto mwenye mwisho miaka 17, zaidi hapo inahitajika vipimo vingine vya afya.

Dr Yacine Zerguini ambaye ni makamu Rais wa kamati ga madaktari wa CAF ambaye pia yupo kwenye bodi ya madkatari wa FIFA amesema asilimia kubwa ya wachezaji kudanganya umri sio maamuzi yao.

Anasema wachezaji wengi wanasaidia na mataifa husika. Ni ngumu kupata cheti feki cha kuzaliwa kama hujasaidiwa na mtu wa serikali. Hivyo shida inaanzia serikalini na sio kwa watoto husika.

Mawakala wengi wa soka wamekuwa na kasumba ya kudanganya taarifa za wachezaji wao kwa lengo la kusaka nafasi za kucheza ulaya.

Lakini sakata hili linazidi kudidimiza fursa kwa wachezaji wetu kupata nafasi kucheza soka la ulaya kwa kuwa tayari vilabu vya ulaya vinajua fika kuwa wachezaji wetu wanadanganya taarifa zao muhimu.

Juzi nilibahatika kukutana na andiko moja kutoka Misri likimnukuu afisa habari wa shirikisho la soka nchini humo Medhat Shalaby likens akisema uongo wa umri wa wachezaji ni kansa inayoteketeza soka la Afrika. Afisa huyo amelaani sana baadhi ya mataifa ya Afrika kudanganya umri hasa katika michuano ya vijana.

Unakuta timu moja imepeleka kweli wachezaji ambao umri wao ni miaka 17 lakini wengine ukiwaangalia unagundua wanalingana umri na akina Essien lakini tunaambiwa wana miaka 16. Kama juzi CECAFA ukiwaangalia wachezaji wa Uganda daah aibu. Yaani sikuona mtoto wa miaka 16 pale. Nani asiyejua maisha ya waafrika?

Mashindano yanapoteza ladha yake maana inakuwa ni michuano ya vijeba na sio vijana tena. Nawapongeza sana Ethiopoa na Tanzania kwa sababu asilimia 80 ya wachezaji wake kweli walikuwa wadogo hata kwa kuwaona tu

Mfungaji bora wa CECAFA raia wa Ethipia

Inawezekana kweli ukidanganya umri unaweza kufanikiwa lakini huko tunakoenda sasa sio dunia ya akina Nwankwo Kanu, Obafemi Martins, Julius Aghahowa, tena. Siku hizi wazungu wamekuwa wajanja sana. Unakumbuka sakata la Samuel Eto’o na kocha wa zamani ea Chelsea, Jose Mourinho alipomsema kuwa alikuwa na umri tofauti una ule aliodai kuwa anao.

Kocha wa timu ya wanawake ya Namibia Jacqueline Shipanga anasema ili soka la Afrika lisonge mbeke kwanza yunapaswa kuwa na sera safi ambazo hazina udanganyifu.


TAARIFA KWINGINEKO AFRIKA

Accra, Ghana


Aliyekuwa bosi wa shirikisho la soka la Ghan Kwesi Nyantakyi ameongezewa marufuku kutoka kwenye kamati ya maadili ya FIFA. Kamati hiyo imeongeza twna siku 45 kabla ya kufanya maamuz mengine.

“Tumeongeza siku nyingine 45, Mr Nyantakyi atakuwa akitumikia marufuku yake ya kutokujihusisha na soka kwa kipindi chote hicho. ”, alisema mwenyekiti wa bodi hiyo.

Nyantakyi alijiuzulu mara baada ya FIFA kumshutumu kwa kupokea rushwa kutoka kwa mwandishi mmoja.


Makala na Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here