Home Kimataifa Bondia Mtanzania aushangaza ulimwengu

Bondia Mtanzania aushangaza ulimwengu

9650
0

Bondia mtanzania Hassan Mwakinyo alieyempiga bondia wa England Sam Eggington katika pambano la utangulizi kabla ya pambano kuu kati ya Amir Khan dhidi ya Samwel Vargas kwa sasa anawataka ma-star wa kimataifa wa mchezo huo.

Mwakinyo (23) kutoka Tanga alishinda pambano kwa Technical Knockout (TKO) dhidi ya bondia mwingereza Sam Eggington kwenye jiji la Birmingham.

Mdau wa masumbwi Chief Juma Ndambile amezungumzia ushindi alioupata bondia Hassan Mwakinyo.

“Amefanya kazi ya ziada ambayo anapaswa kupongezwa na kila mdau wa ngumi, bondia aliyepigana nae ni mkubwa sio wa kubeza kama watu wanavyofikiria labda ni bondia wa kawaida. Kwa uzito wao, Sam Eggington ni bondia namba 8 duniani na namba 2 ndani ya England, bondia wetu (Hassan Mwakinyo) alikuwa namba 174 duniani na namba moja Tanzania.”

“Bondia aliyepigwa na Mwakinyo kwa profile yake hakuamini kama anaweza kupigwa na Mwakinyo kwa sababu amepigana mapambano mengi sana na amekuwa bingwa mara tatu wa WBC, huo ni mkanda mkubwa sana duniani.”

“Tunapaswa kumuunga mkono, baada ya kumpiga tu mabondia wakubwa wamejitokeza kama Kerry. Tungekuwa na mipango endelevu tungeandaa mazingira pambano hilo liwe Tanzania kwa sababu anapopigana mbele ya mashabiki wake atafanya vizuri zaidi.”

“Mabondia ambao anafikiria kupigana nao kwa sasa ni pamoja na Amir Khan kwa sababu ndio uzito wake hata Floyd Mayweather ndio uzito wake kwa hiyo unaweza kusikia anapigana nae kwa sababu wanauzito sawa.”

“Endapo atapigana na Kerry au Amir Khan ni hatua kubwa katika ulimwengu wa ngumi za kulipwa. Ombi langu kwa Waziri na serikali kwa ujumla ni kumpa support sana ukizingatia amekuwa akipambania michezo yote kwa ujumla.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here