Home Kimataifa Mtanzania Dominicusius Kuhanga anayekipiga Zimbabwe apata shavu Botswana

Mtanzania Dominicusius Kuhanga anayekipiga Zimbabwe apata shavu Botswana

11828
0

DOMINICUSIUS KUHANGA ni mtanzania ambaye kwa sasa yupo katika akademi ya vijana ya Aces ya nchini Botswana.


Kuhanga ni nani?

  • KUHANGA amezaliwa 27 Nov 2000
  • Alizaliwa na kukulia mkoani TABORA, TANZANIA

Soka lake alianzia wapi?

  1. KAISERS FC (Tabora 2012-14)

  2. CHIPUKIZI ACADEMY ( Tabora 2014)

  3. MARA SPORTS ACADEMY (Musoma 2015-2017)


Pia aliiwakilisha Tabora katika mashindano ya Copa coca Cola U-15 mwaka 2013 na 2014


Safari yake ya Zimbabwe?

“Nilikuja Zimbabwe mwenyewe Tarehe 22 Desember 2017 kwa ajili ya kufuata nyayo za (Khama Billiat) ambaye alianzia soka lake AYSA na nilisafiri kwa kutumia ada ya shule niliyopewa na bibi yangu. Baada ya kufanya majaribio wakaamua kunisaidia ingawa huku kuna ubaguzi sana wa utaifa hasa kwenye hizi akademi zao kwani lengo ni kwa vijana wa Zimbabwe tu.Vipi kuhusu Safari yake ya Mafanikio?

Alipewa ruhusa na uongozi wa akademi baada ya wao kupata habari juu ya majaribio ambayo yalikuwa yakifanyika mjini Gaborone. Uongozi wa akademi hiyo ukashughulikia mchakato mzima wa safafi yake ikiwa ni pamoja na tiketi ya basi kutoka Harare mpaka mjini Gaborone.Majaribio yalikwenda vipi?

“Nilifika salama na wakanipokea vizuri na siku iliyofuata majaribio yalikaanza pale NOTWANE GROUNDS, nje ya uwanja wa taifa wa Botswana”


Majaribio hayo yaliandaliwa na klabu ya Notwane FC ya nchini Botswana inayoshiriki ligi daraja la kwanza

Majina Notwane Football Club
Utani Sechaba,Makhete, Toronto,
Team e Bosisi
Kuanzishwa 1965
Uwanja Botswana National Stadium
Gaborone, Botswana
Uwezo watu 22,500
Ligi Botswana First Division

Notwane imewahi kutwaa mataji matatu ya ligi kuu Botswana .


Mwenendo wa Majaribio ulikuwaje
“Tulikuwa vijana 170 wa umri kuanzia miaka 17 na kuendelea”


“Majaribio yalikuwa ya siku 3 tu hivyo tulicheza dakika 10 ili kupunguza idadi na tuliochaguluwa tuliendelea na hizo siku 2 zilizobaki ambapo mimi nilifanikiwa kubaki katika watu 12 tuliofuzu majaribio hayo huku mimi nikiwa mchezaji pekee wa kigeni kubaki na nilikuwa mchezaji mdogo kuliko wote aliyepata fursa ya kubaki (17)”


Nikamuuliza kama ana miaka 17 kwanini hakuitwa timu ya taifa ya vijana ya Serengeti?

“Serengeti waliita wale waliozaliwa 2002 na tu, mimi umri ulikuwa miaka 17 na miezi kadhaa hivyo sikuweza kupata nafasi hiyo labda Ngorongoro heroes”Je baada ya kubaki sasa vipi suala la mkataba na Notwane?
“Kutokana na sheria za FIFA wakashindwa kunipa mkataba na wakawasiliana na akademi yangu juu ya mimi kwenda kukamilisha mkataba huo mwezi November ambapo nitakuwa nimetimiza miaka 18”Je ukiachilia mbali Notwane kuna harufu yeyote ya vilabu vingine?
“Ndio, kuna kiongozi wa Gilport Lions FC ( Mr. JETHRO HUNIDZARIRA ) ya ligi daraja la kwanza Botswana alichukua mawasiliano yangu baada ya kuvutiwa na kiwango changu, hivyo ni suala la muda na maslahi ya kimkataba”


Ukitaka kusoma makala yake niliyoandika hapo awali kuhusiana na maisha yake ya soka Click/Bonyeza hapa

Makala na Privaldinho ( Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here