Home Kitaifa Mtazamo wa Shaffih Dauda kuhusu ligi kukosa mdhamini na nini kifanyike

Mtazamo wa Shaffih Dauda kuhusu ligi kukosa mdhamini na nini kifanyike

9663
0

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limekiri kwamba hadi sasa haijulikani bingwa wa ligi kuu Tanzania bara atapata zawadi gani baada ya aliyekuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kujiweka pembeni hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema, pamoja na hayo TFF bado ipo kwenye mazungumzo na makampuni mbalimbali nchini kuhakikisha kwamba bingwa anapata zawadi inayostahili kulingana na ligi husika.

Kwa mujibu wa takwimu ambazo zipo katika nchi 5 Afrika zinazoongoza kwa wananchi wake kupenda na kufatilia mchezo wa mpira wa miguu Tanzania ipo ukiachana na nchi kama Misri, Tunisia na Afrika Kusini na huo ni wa ujumla.

Ndani yake kuna kitu tunaita local content elevance (mashabiki kupenda soka la ndani) kwa sababu inawezekana kabisa nchi ikawa inafatilia masuala ya soka lakini ni nje ya nchi, lakini Tanzania inaendelea kubaki kuwa miongoni mwa nchi ambazo mashabiki wake pamoja na kupenda timu za nje lakini bado wanapenda mpira wa nyumbani.

Sasa ni kitu gani ambacho kinafanya makampuni yashindwe kuona hiyo fursa? Kwa utafiti wangu kuna tatizo katika pande zote mbili. Makampuni hayaoni fursa kwa sababu hawaangalii katika nyakati tulizonazo sasa hivi. Kwa mfano wanafikiri wakidhamini ligi halafu ligi ikapewa jina la bidhaa yao (Shaffih Premier League) tayari inatosha kwao kupata wanachostahili kupata.

Mimi fursa ninayoiona ambayo pia siamini kama hawa partners wengine hawajaiona. Kwa mfano kampuni ya vinywaji baridi, bia au mtandao wa simu pamoja na wenye ligi (Bodi ya Ligi na TFF) wanatakiwa kuangalia ni wapi ambapo kila mmoja atanufaika.

TFF na Bodi ya Ligi wanamuhitaji partner aje kuwapa wepesi wa kuendesha ligi kwa maana ya kuziwezesha timu, gharama za uendeshaji pamoja na zawadi lakini huyu partner yeye ananufaikaje? Sasa hapa ndio penye ishu ambayo mimi binafsi nashindwa kuelewa.

Kwa mfano kampuni ya bia inashindwaje kuiona hiyo fursa ya kuingia kwenye mpira ikiwa wao biashara yao kubwa ni kuuza? Wakati huohuo mchezo wa mpira wa miguu ni starehe kwa hiyo huwezi kuutenganisha na bia.

Kinachotakiwa ni wao kuona namna gani ya ku-focus kwenye soko la mpira. Nakupa mfano, kunaweza kuwa na activation ambazo zinafanyika viwanjani kabla na wakati wa mechi husika. Juzi kati nilikuwa Mwanza kwenye mechi ya Mtibwa na Simba sehemu ya timu ya Sports Xtra ilikuwa Kanda ya Ziwa wiki moja kabla ya mechi, siku ya mechi Kirumba imetapika watu.

Lakini ishu haikuwa watu waliojaa CCM Kirumba kwa ajili ya kuingia kwa sh. 5000, mzunguko wa kibiashara pale Mwanza ulikuwa ni mkubwa mno, nikajiuliza ingekuwepo official beer wanakamata hiyo fursa ya uwepo wa wageni zaidi ya 50,000 pamoja na wazawa halafu wakawa na promotions zao kwa ajili ya ku-push volume ya bia zao wakatengeneza mobile bars pale Kirumba ambapo mashabiki wanapata bia, soda na vyakula.

Tatizo wadhamini wetu bado wanatazama kwenye mileage pekeake kuliko activities zitakazowafanya wauze moja kwa moja. Kila siku huwa nazungumza na bado nitaendelea kusimamia hapohapo ni kwamba, miongoni mwa matatizo makubwa yanayotukabili ni kutoruhusu watu walibobea katika eneo fulani kuachwa wafanye jambo hilo, nimefanya tafiti na nimejiridhisha.

Watu wanataka kukumbatia mambo na kufanya wenyewe wakati hawana uwezo na maarifa ya kufanya jambo hilo, mwisho wa siku huwezi kufanikiwa. Tuachane na mazoea kwamba tukienda kwenye mpira ni mechi tu uwanjani. Tusipambane kuwashawishi watu kuja uwanjani halafu matokeo yake wanaishia kuangalia mechi, mtu akija uwanjani lazima atengenezewe excitement lazima kuwe na entertainment element.

Kwa makampuni ya simu kwa takwimu zilizopo, wnasema watanzania ni watumiaji wazuri wa internet, watu wanahitaji taarifa kupitia kiganjani. Siku hizi uki-post magoli ya ligi ya Bongo ukiangalia vieweship ni tofauti na kitu kingine chochote. Kuna fursa ya kuangalia watu wangapi wanaotumia internet katika population ya Tanzania na kutengeneza package na product kwa sababu watu wanapenda kuangalia highlights na magoli si watu wote wanaangalia kupitia TV au wanakuwepo uwanjani.

Kampuni ya simu ambayo ni tayari partner wa ligi wanaweza kutengeneza online content watu waka stream.

Upande wa pili (Bodi ya Ligi) na wao lazima wafanye kazi yao kwa maana ya ku-brand ligi, hii ni bidhaa lakini ili iwe bidhaa kuna namna inatakiwa ifanyike ili mteja aweze kuikubali bidhaa yako na ikubalike kwenye soko. Ligi bado haijawa branded.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here