Home Uncategorized Mtazamo wa Shaffih Dauda kuhusu Messi kupigwa chini tuzo za mchezaji bora...

Mtazamo wa Shaffih Dauda kuhusu Messi kupigwa chini tuzo za mchezaji bora wa FIFA

12205
0

Lionel Messi kapigwa chini kwenye tuzo ya mwanasoka bora wa dunia ‘The best FIFA Men’s Player of the Year’ Lionel Messi, katika fainali ya kuwania tuzo hiyo wameingia walewale walioingia fainali kwenye tuzo ya mchezaji bora wa UEFA (Ronaldo, Salah na Modric)

Kwa nini Messi hayupo?

Kwa mtazamo wangu, Messi alitakiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA.


Messi anachukua nafasi ya nani kati ya Salah na Ronaldo?

Kwa mtazamo wangu, Salah hakutakiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watatu waliofika fainali. Moja kwa moja namtoa Salah nafasi yake namuweka Messi.

Mo Salah alikuwa na msimu mzuri akiwa na Liverpool, haipingiki alifunga magoli 43 katika msimu na alikuwepo kwenye fainali za kombe la dunia akaishia hatua ya makundi. Ameisaidia Liverpool kufika fainali ya Champions League hawakushinda taji, kwenye EPL pia hakushinda taji.

Why Messi?

Alifunga mabao 44 katika msimu uliopita, aliiongoza Barcelona kushinda mataji mawili (Copa del rey na La Liga). Fainali za kombe la dunia hazikuwa nzuri kwa Argentina walitolewa na Ufaransa hatua ya 16 bora. Messi aliisaidia Argentina kufika hatua ya mtoano ukilingalisha na Salah.


Sina wasiwasi wala shida kwa Luca Modric na Ronaldo (mfungaji bora-UEFA Champions League) ambao walifanya vizuri kwenye Champions League. Mashindano ya Champions League yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa kwenye tuzo ya mchezaji bora wa dunia kutokana na profile na ukubwa wa tournament yenyewe.

Hayo ni mawazo yangu, na wewe una mawazo yako, niandikie comment yako Messi alipaswa kuwepo kwenye tuzo hii? Kama Ndio kwa nini? na kama Siyo kwa nini?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here