Home Kitaifa Mtibwa Sugar yaokoa kipaji cha Razak Daiva, chipukizi aliyesuswa Azam FC

Mtibwa Sugar yaokoa kipaji cha Razak Daiva, chipukizi aliyesuswa Azam FC

12735
0

Mtibwa Sugar ni moja ya klabu kongwe kabisa ndani ya ligi kuu Tanzania. Ni klabu ambayo sera yao ni kuinua viwango vya wachezaji wachanga kama akina Ramadhani Shiza Kichuya n.k

Klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani morogoro hivi majuzi iliandaa majaribio ya kupata vijana wenye uwezo ndani ya jiji la Dar ss Salaam. ilifanikiwa kuwanasa wachezaji watatu katika harakati ya kuimarisha kikosi chao.


Wachezaji hao ni nani na nani?

Golikipa Razak Daiva golikipa wa zamani wa Azam Fc ya vijana, Omary Ally Malungu a.k.a Van Magoli ambaye ametokea akademi ya Mabibo FF ya hapahapa Dar es Salaam.

Makala yetu leo tunaanza na Razak Daiva.

Daiva ni nani?

Ni mzaliwa wa Tanga. Soka lake alianzia Tanga. Alianzia kufanya mazoezi na klabu ya Mgambo Shouting ambayo ilikuwa inafanya mazoezi yake uwanja wa mizani karibu na nyumbani kwake uliopo maeneo ya Kange.

Baada ya hapo akajiunga na akademi ya Veterani. Pia alishiriki michuano iliyoandaliwa na Azam akiwa anaitumikia klabu ya Makolola Star. Mchezo wa kwanza walishinda 3-2, mchezo wa pili wakacheza na Azam na kuwafunga 4-2 na wakafanikiwa kutwaa ubingwa huo.

Je harakati zake ziliishia hapo?

“Tukarudi tena Tanga, lakini niliamua kurudi klabu yangu ya zamani (Veteran) kwa sababu Makolola walinichukua kwa muda tu” Razak

“Baadae Makolola wakaniomba tena niwachezee ligi ya mkoa, msimu wa pili nikarudi tena Veterani nikacheza tena ligi ya mkoa, baadae Coastal Union wakaniona wakanichukua, nikacheza msimu mmoja lakini kwa bahati mbaya ikashuka daraja”

“Baada ya kuonesha kiwango kizuri msimu wa 2014/15 kocha Mwanatwa Kiwelo akiunganisha na Mwadui nikaenda kucheza Timu B”

Lakini baada ya kwenda Mwadui alikumbana na changamoto kubwa ya muda kwani wakati huo huo alikuwa anasoma kidato cha 4 shule ya Sekondari Usagara hivyo hakubatika kusajiliwa timu ya wakubwa kule Mwadui.

Baada ya kumaliza shule akarudi tena mwadui na akashiriki kombe la Uhai Cup kule Bukoba na Simba walitwaa ubingwa huo 2016/2017. Mwadui walishikilia mkia kwenye kundi letu lakini sikubahatika kucheza pia kwasababu nilikuwa bado sijasajiliwa.


Safari ya Azam ikaiva

Baada ya hapo klabu ya Azam ilimuona na kumchukua kwenye akademi yao. Msimu wake wa mwisho aliichezea Azam Fc kwa msimu mmoja ambao alimalizana naomwaka huu.

Changamoto alizokutana nazo Azam?

Hakubahitika kushiriki michuano ya uhai Cup baada ya kuumia goti. Lakini pia aliwahi kushiriki michuano ya East Afrika Cup. Lakini katika michuano hiyo ya East Afrika Cup walitolewa na klabu ya Msimamo hatua ya Robo fainali kwa mikwaju ya penati.

Kwanini aliondoka Azam Fc?

“Baada ya kusumbuliwa na majeraha sana Azam walionesha nia ya kutokuendelea na mimi. Nikawa muda mwingi naenda kufanya mazoezi na akademi ya Mabibo FF”

Asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi chety wote waliondoka baada ya mwalimu wetu wa hapo awali kuondoka pia. Mpaka sasa kwenye kikosi cha wachezaji 24 tuliokuwa nao wamebaki wanne tu kwenye kikosi chao cha sasa.

Safari yake ya Mtibwa vipi?

Niliposikia Mtibwa wanatafuta vipaji nikajaribu tena bahati yangu. Walikuwepo wacheza 200 na walitaka wachezaji kadhaa tu. Kati ya wachezaji hao 200 tulibaki wachezaji watatu tu, mimi (Razak) na wachezaji wawili wa akademi ga Mabibo FF (Omary Malungu Van Magoli)

Kwa sasa anaitumikia mtibwa baada ya kusaini mkataba wa miaka kadhaa na atakuwa kwenye kikosi cha vijana wa miaka 20.

Kila la kheria kwake


Makala na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here